Serikali imeiagiza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kuhakikisha
inajipanga kwa ajili ya kuboresha Viwanja vya Mwanza na Kilimanjaro
ili kuweza kukabiliana na ongezeko kubwa la abiria watakaokuwa wakitumia
Viwanja hivyo, baada ya Safari Za Ndege ya Fastjet kuanza.
Agizo hilo limetolewa leo na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles
Tizeba, wakati akiizundua Ndege ya Shirika la Ndege la Fast Jet jijini
Dar es Salaam.
'Nawaagiza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kuhakikisha
kuwa wanaviandaa Viwanja vya Mwanza na Kilimanjaro kwa ongezeko la Abiria
ambao wanategemewa kutumia Viwanja hivyo. Ni matumani yangu Mamlaka
inalichukua swala hili kwa umuhimu wake na itahakikisha kuwa hakuna
Abiria atakaeshindwa kusafiri kwa sababu ya msongamano wa Abiria katika
Viwanja Vyetu', Alisema Dk Tizeba.
Aidha Dk. Tizeba aliongeza kama sehemu ya jitihada za Serikali kuboresha
Mazingira ya Sekta ya Usafiri wa Anga. Serikali imeweka mazingira mazuri
kwa sekta binafsi kuwekeza katika ujenzi wa Miundombinu ya Viwanja Vya
ndege.
"Serikali imeweka mazingira mazuri kwa sekta binafsi kuwekeza
katika ujenzi wa Miundombinu ya Viwanja Vya ndege ambayo inakwenda sambamba
mabadiliko ya sheria na maboresho ya kanuni'. alisema Dk. Tizeba.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la fastjet amesema
siku ya leo ni siku muhimu sana si kwa Shirika hilo lakini pia na kwa
Tanzania na Afrika maana usafiri wa bei rahisi umezunduliwa.
"Leo ni siku muhimu sana kwa Shirika la fastjet, Tanzania na
Afrika kwa ujumla. Kwa Muda mrefu waafrika hawakuwa na usafiri wa Anga
wa Uhakika na wa kuaminika .Fast jet itawawezesha kutumia usafiri wa
Ndege na Shirika linatarajia kuwahakikishia usafiri wa bei nafuu kutoka
sehemu moja kwenda nyingine'.alisema Bw. Edward.
Edward aliongeza mpaka saa Shirika limeshaajiri watanzania 70 ambapo
miongoni mwao ni Wahudhumu wa Ndege(Vabin Crews), na watu wa masoko
na akaongeza kuwa kampuni itaendelea kuajiri watanzania wengi kadri
Shirika litakavyoongeza Ndege zake.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania (TAA), Mhandisi. Suleiman S. Suleiman amesema Mamlaka imejipanga
kwa ajili ya kuboresha Sehemu za kusubiria Ndege na imeahidi kuendana
na Mahitaji ya yanayotakiwa.
Shirika la Ndege la fastjet litaanza safari zake Tarehe 29 Novemba
2012 kwa safari mbili kila siku ambazo ni Kuanzia Dar es Salaam-Mwanza
na Dar es Salaam-Kilimanjaro.Nauli ya chini kabisa inakadiriwa
kuwa Kiasi cha hilingi za kitanzania 32,000/- na Tiketi ya Juu kabisa
inakadiriwa kuwa Shilingi za Kitanzania 92,000/- bei hizo zikiwa bila
vat.
Lengo la Shirika hili ni kuvutia abiria wengi zaidi hasa wale wa kipato
cha kawaida kuweza kutumia usafiri huo. Na kiwango cha Nauli ni kidogo
ili kuwavutia wale ambao hawajawahi kutumia usafiri huo wautumie.
Toa Maoni Yako:
0 comments: