Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simu za Mkononi, Sam Elangalloor, wakifunua kitambaa kwa pamoja kuashiria uzinduzi wa Shule ya Msingi Kiromo, iliyopo Wilaya ya Bagamoyo-Mkoa wa Pwani, iliyokarabatiwa na Kampuni ya Airtel Tanzania. Uzinduzi huo umefanyika
leo Nov 27, 2012.
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simu za Mkononi, Sam Elangalloor, wakati akionyeshwa madawati yaliyotolewa na Kampuni hiyo kwa Shule ya Msingi Kiromo, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Shule hiyo baada ya kukamilika kwa ukarabati. leo
Nov 27, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simu za Mkononi, Sam Elangalloor, kuhusu matumizi na makusudio ya mafunzo ya Kompyuta wakati alipotembelea katika chumba cha Kompyuta, baada ya kuzindua rasmi shule ya Msingi, Kiromo, leo Nov
27, 2012.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simu za Mkononi, Sam Elangalloor, kukagua maeneo ya Shule ya Msingi Kiromo, wakati wa hafla ya uzinduzi wa shule hiyo, uliofanyika leo Nov 27, 2012, shuleni hapo baada ya kukamilika kwa ukarabati uliofanywa na
kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel Tanzania.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Sam Elangalloor, wakati alipokuwa akitembelea katika Chumba cha Maktaba cha Shule ya Msingi Kiromo, baada ya uzinduzi rasmi wa shule hiyo, uliofanyika leo Nov 27, 2012.
---
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imezindua shule ya msingi kiromo iliyopo bagamoyo mkoa wa pwani baada kuijenga upya shule hiyo nakuipatia vifaa bora vya kufundishia kwa lengo la kutoa mazingira mazuri ya wanafunzi kujisomea

Ujenzi wa shule ya kiromo ni mwendelezo wa dhamira ya Airtel kupitia mradi wake wa "Airtel shule yetu" wenye lengo la kushirikiana na serikari kuhakikisha wanaweka mazingira bora katika utoaji wa elimu kwa kujenga majengo, kutoa vifaa vya kufundishia pamoja kutoa udhamini wa masomo kwa wanafunzi.

Akiongea wakati wa halfa ya uzinduzi iliyofanyika shuleni hapo, Mkurugenzi Mkuu wa Airtel  Bw, Sam Elangollor alisema "tulianzisha mradi wa Airtel shule yetu kwa lengo la kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha utoaji wa elimu kwa wavulaa na wasichana, tulianza na shule ya Kiromo ikiwa na hali mbaya sana, madarasa yote yalikuwa yameharibika vibaya huku asilimia 80 ya wanafunzi  wa  umri kati ya miaka 7-13 wakikaa chini "Airtel tumerekebisha majengo yaliyokuwepo na kisha kujenga majengo mapya ya madarasa, ofisi kwaajili walimu, maktaba ya shule, darasa la komputa pamoja na jiko kwaajili ya chakula cha mchana kwa wanafunzi" aliongeza bw Ellangaloor.

Vile vile "Airtel tumeweka umeme katika shule hii mara baada ya kuijenga na kuhakikisha tumeweka madawati katika madarasa yote, vitabu vya kutosha katika maktaba, komputa zitakazotumika kwa ajili ya kujifunza somo la kompyuta na kuunganishwa kwenye mtandao wa internet, aliendelea kusema mkurugenzi huyo Airtel tunatambua jitihada za serikali yetu katika kuhakikisha inatoa misingi ya elimu bora  ili kufikia lengo la Milenia ingawa bado kunachangamoto nyingi katika kutoa elimu bora.  Ni imani yetu kupita mradi wetu wa "Airtel shule yetu" tutamuwezesha mtoto wakitanzania kupata elimu bora kwa kuwawekea misingi ya uraia bora na kuchangia katika uchumi wa nchi yetu Alimaliza kusema bw Elangalloor.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo  mgeni rasmi Mheshimiwa Makamu wa Raisi  Ghalib Bilal  alifafanua kuwa "Kitu pekee ambacho kinatofautisha nchi zilizoendela na zinazoendelea sio utajiri na malibali ni elimu. Hii ni kwasababu utajiri na mali havijileti vyenyewe isipokuwa huchochewa na maendeleo mazuri ya msingi wa ELIMU"

hivyo kwakuzingatia hilo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunaishukuru sana Airtel Tanzania kwa kutuunga mkono katika dhamira yetu ya kuwekeza katika sekta ya elimu nchini kwa kujenga na kukarabati shule hii ya Kiromo pamoja na kuwa mstari wa mbele katika kujitolea katika kutoa vitabu kwa shule mbalimbali nchini.

"Napenda kuwashukuru walimu , kamati ya shule,  pamoja na wizara ya elimu kwa kushirikiana na Airtel katika kuhakikisha ujenzi  wa shule hii umekamilika" aliongeza Mheshimiwa  Makamu wa raisi.

Airtel Tanzania imejiwekea mikakati ya  kusaidia maendeleo ya jamii hususani elimu ya msingi na sekondari kwa kuwa ndio msingi wa mwanzo kabisa katika mfumo wetu wa elimu

Kupitia mradi wa  "Airtel shule yetu"  zaidi ya shule za sekondari 1000 zimefaidika kwa kupatiwa vifaa vya kufundishia  vikiwemo vitabu na madawati. Pia Airtel Tanzania inatoa udhamini kwa kulipia gharama za masomo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa wasichana na wavulana ambapo hadi leo hii  Airtel inajumla ya wanafunzi  watano wanaosoma elimu ya juu kwa kulipiwa gharama zote  za masomo huku wengine 34 wameshamaliza na wameajiriwa katika makampuni mbalimbali nchini ikiwemo Airtel.

Mradi wa shule yetu  (Adapt the school) ni mpango unaoendeshwa na Airtel katika nchini zote 20 za Afrika.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: