11/01/2012 - 12/01/2012
Bwana Harusi Richard Mllatie Assey akimvisha pete mkewe Bibi. Jacline Hamson Ghikas wakati wa ndoa takatifu illiyofungwa leo jijini Dar es Salaam katika kanisa la St. Peters.
Maharusi wakipigana busu bashasha baada ya kuvishana pete.
Bwana Harusi Richard Mllatie Assey akiangusha saini katika gamba la kuhalalisha ndoa takatifu.
Bibi Harusi Jackline Richard Mllatie Assey naye akitia saini.
Maharusi wakionyesha vyeti vya ndoa.
Wapambe wa maharusi wakati wa ibada ya ndoa takatifu,
Wazazi wa Maharusi Mr & Mrs Assey na Mama mzazi wa Bwana harusi wakionyesha furaha baada ya watoto wao kufunga ndoa.
Pichani juu na chini baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki waliofika kushuhudia ndoa takatifu ya Bwana na Bibi Richard Mllatie Assey.
Bwana na Bibi Harusi Richard Mllatie Assey na Jackline Hamson Ghikas wakitoka kaniasani baada ya kufunga ndoa takatifu katika kanisa la St. Peters Oysterbay jijini Dar.
Wakionyesha nyuso za Furaha baada ya kuhalalisha ndoa yao
Bwana Harusi Richard Mlatie Assey na mpambe wake wakishine na Suti matata zilizobuniwa na Sheria Ngowi,
Wapambe wa maharusi katika pozi,
Wapambe wakiume ndani ya suti zilizobuniwa na Sheria Ngowi.


MMILIKI wa gari ambalo lilikuwa likiendeshwa na msanii maarufu nchini, Hussein Ramadhan ‘Sharo Milionea’ na kupata nalo ajali iliyosababisha kifo chake huko Muheza, Tanga, Mohammed Ismaili maarufu kwa jina la Mudi Suma, ameibuka na kueleza uhusiano wake na marehemu, huku akisema amekubali hasara.
 
Akizungumza kwa simu kutoka Muheza jana Suma alisema hana mpango wa kudai fidia au kupeleka malalamiko yoyote kwa ndugu wa marehemu kwa kuwa; “Kilichotokea ni kazi ya Mungu.” “Siwezi kudai hata kidogo hivyo ni vitu vya kupita tu. 

Marehemu alikuwa ni zaidi ya ndugu yangu, gari ni kitu kidogo sana katika uhusiano tuliokuwa nao,” alisema Suma na kuongeza kwamba hata Marehemu Sharo Milionea naye alikuwa amemwachia mali zake kadhaa ikiwamo gari. “Siyo gari tu alilokuwa ameniachia. Kuna mikataba yake ya kazi, Bajaji yake na funguo za chumbani kwake. Nasubiri kukabidhi vitu hivyo baada ya kukaa na ndugu zake. Vitu viko kwenye mikono salama,” alisema.
Kuhusu gari lake lililopata ajali, Suma alisema lilikuwa na bima ndogo, lakini anapanga kwenda TRA atakaporejea Dar es Salaam kufuatilia baadhi ya mambo.
“Kabla ya kuondoka bima ile kubwa ilikuwa imekwisha kwa hiyo nikaamua kuikatia bima ndogo. Nitakapofika kesho (leo) Dar es Salaam, nategemea kwenda ofisi za bima kuzungumza nao,” alisema Suma. Alipoulizwa kama kuna mtu mwingine atakayeathirika kutokana na gari hilo kuharibika katika ajali mbali na yeye, alijibu: “Hakuna tofauti na mimi mwenyewe na familia yangu.”

 Kabla ya ajali.  
Suma alieleza kuwa kabla ya kuanza safiri yake, Sharo Milionea alifika nyumbani kwake mchana na kumweleza kuwa afya yake haikuwa nzuri. “Kabla ya kuondoka aliniambia kuwa hajielewi elewi na kifua kilikuwa kinambana. Nikamshauri asiondoke peke yake, atafute mtu wa kuondoka naye ambaye atamsaidia kuendesha gari njiani,” alisema Suma na kuongeza:
“Tulianza kuwapigia simu jamaa zetu wanne wa kusafiri naye lakini kila tuliyemwambia hakuwa tayari. Ilikuwa ni changamoto mpaka ilipofika saa 10:45 hivi jioni, akaamua kuondoka peke yake. Wakati anatoa gari getini kwangu, nikamwambia, basi jaribu kuwa mwangalifu sana, maana alikuwa kweli anasumbuliwa na kifua. Tukakubaliana kwamba atakaporudi aende hospitali kucheki afya yake.”
Kuhusu uhusiano wake na marehemu, Suma alisema: “Mimi ni mfanyabiashara na yeye alikuwa msanii, lakini ilitokea tukawa marafiki sana mpaka ikafikia wakati nikaona kuwa ni ndugu yangu. Nilimwamini nikamtambua kama sehemu ya familia.”
Alisema marehemu alikuwa akitumia gari hilo kila alipolihitaji na safari ya kwenda nalo Tanga kwa wazazi wake ilikuwa ni ya tatu.“Siyo mara ya kwanza kuitumia gari lile, nilikuwa nimemwamini sana. Safari ya kwanza alichukua na kusafiri nalo mwenyewe, halafu safari ya pili ikafuata na hii ilikuwa safari ya tatu,” alisema Suma.
Eneo la ajali wakimbia makazi Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Songa Kibaoni mahala ambako Sharo Milionea alipatia ajali, wamezikimbia nyumba zao baada ya Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Subira Mgalu kutoa siku moja kwa waliopora mali za marehemu huyo kuzisalimisha mara moja.
Hili ni moja ya soko linaloshamili kwa kazi sana jiji Dar es Salaam (lipo Buguruni relini) japo serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imelifumbia macho si salama kwa afya za binadamu na usalama kwa ujumla. Napenda kusema kuwa watendaji wetu wameshindwa kukomesha na kuliondoa kabisa mambo mbali mbali yanayoendelea kinyume cha sheria. ANGALIZO: Mamlaka muhimu ni vyema ikachukua sheria muhimu kuzuia hali hii inayotokea ili kuepusha majanga yanayotokea mbeleni.
Washiriki wa shindano hilo wakiwa katika pozi la pamoja.
Meneja matukio wa Dar Live, Abdallah Mrisho, akielezea namna burudani zitakavyopamba za kesho ndani ya ukumbi huo.


Baadhi ya waandishi wa habari na washiriki wa shindano hilo wakisikiliza ufafanuzi wa waandaji wa mchakato huo.


Mratibu wa shindano la The Mic King, Luqman Maloto (katikati), akielezea kwa ufasaha mchakato wa kuwapata washiriki hao ulivyofanyika.
Washiriki wakisikiliza kwa makini utambulisho wao kwa wanahabari leo.

Wanahabari wakichukua matukio wakati wa utambulisho huo.

Washiriki wa shindano hilo wakiwa katika pozi la pamoja.
---
WASHRIKI wa shindano la The Mic King linaloratibiwa na uongozi wa Ukumbi wa Taifa wa Burudani wa Dar Live, leo wametambulishwa rasmi kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya hapa nchini.

Utambulisho huo umefanyika ndani ya Ukumbi wa The Atriums Hotel iliyoko Sinza-Afrika Sana jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mratibu wa Shindano hilo, Luqman Maloto, alisema amelazimika kutoa utambulisho huo leo kwa kuwa kesho washiriki hao watachujwa ndani ya Ukumbi wa Dar Live kwa mara ya kwanza tangu walipoingia kwenye

Top 20.
Maloto amewaomba mashabiki wa burudani waje kwa wingi kesho ndani ya ukumbi huo ili waweze kujipatia fursa ya kumchangua mkali katika shindano hilo ambalo fainali zake zinatarajiwa kufanyika Machi mwaka ujao.
Pia meneja matukio wa Dar Live, Abdallah Mrisho, amesema kesho katika utambulisho huo kutakuwa na shoo ya nguvu inayofahamika kwa jina la Usiku wa Wanyama, ambapo wasanii kibao mashuhuri watatumbuiza.
(Habari/Picha: Musa Mateja/GPL)
Bi. harusi mtarajiwa Bi. Dorice Aloyce Tendewa akiwa katika pozi meza kuu wakati wa tafrija maalum ya kumuaga na kumtakia kila la heri katika maisha yake mapya ya ndoa ambayo anataraji kuifunga Jumamosi ya Desemba 1, 2012 katika Kanis la KKKT Usharika wa Azania Front jijini Dar es Salaam. Tafrija hiyo iliyofana sana ilifanyika katika ukumbi wa New Msasani Beach Club.
 Bi. Dorice Tendewa, Biharusi mtarajiwa (kushoto) akiwa na msimamizi wake na
rafiki yake mkubwa, Betha Mwakapenda wakati wa tafrija yao maalum ya
kumuaga. 
 
 Bi.Dorice Tendewa akisaidiana na Msimamizi wake, Bi. Betha Mwakapenda kukata keki.
  Bi Harusi Mtarajiwa Dorice Tendewa akitambulisha wageni mbalimbali ndugu zake kwa wageni waliofika katika tafrija yake
Picha ya pamoja ya familia nzima ya Bwana na Bibi Aloyce Tendewa. KWA PICHA ZAIDI BOFYA FATHER KIDEVU BLOG
 Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde na Msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo flava) kwa pamoja wakionyesha tuzo ya  Channel O  aliyoipata Mwanamuzi huyo nchini Afrika Kusini. Tukio hilo limefanyika leo wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo Airtel imempongeza AY kwa ushindi alioupa pamoja na kumwandalia sherehe ya kumpongeza itakayofanyika leo usiku nyumbani Lounge jijini Dar es Salaam 
Afisa Uhusiano wa Airtel akiongea wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo Airtel imempongeza AY balozi wake kwa kupata tuzo ya chanel O ya video bora, Katikati ni AY  akifatiwa na DJ wake Athur Baraka
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo flava)  na Balozi wa Ambwene Yessaya 'AY'
Msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo flava)  na Balozi wa Ambwene Yessaya 'AY' akiwashukuru watanzania kwa kumpigia kura na kumwezesha kupata tuzo hiyo kulia ni Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde na kushoto ni  DJ wake Athur Baraka.
--- 
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel wakiwa na balozi wake Ambwene Yessaya “AY” leo wamewashukuru watanzania kwa kumpigia kura msaani maarufu wa kizazi kipya Ambwene Yessaya  “ AY “  na kumwezesha kuibuka mshindi wa tuzo ya kwanza katika kipengele cha Most Gifted East African video of the Year kupitia kibao chake kipya kijulikanacho kama “I don’t wanna be alone”
Akiongea na wandishi wa habari katika Ofisi za Airtel leo AY amechukua fulsa kuwashukuru watanzania kwa kumpigia kura na kuweza kumwezesha kuibuka na ushindi. Aidha alivishukuru vyombo vya habari kwa kuendelea kushirikiana naye katika kufikisha habari na kumsaidia kupata tuzo hiyo.
Naye Afisa uhusino wa Airtel Jane Matinde alisema” tunafurahi kuona msanii AY ambaye ni balozi wetu kuibuka na tuzo iliyoshirikisha wasanii mbalimbali toka  Afrika, sisi tunasikia furaha kuona mafanikio ya wasanii wetu nchini yakiendelea kukua na ndio sababu leo tuko hapa kusherehekea ushindi  huu kwa pamoja na kuwashukuru watanzania kwa kumuwezesha AY kupata tuzo hii kwa kura zenu.
Tunapenda pia kuchukua fulsa hii kuwaalika watanzani na wateja wetu leo pale nyumbani lounge usiku kuanzi saa tatu tuweze kujumuika na AY na kumpongeza kupata tuzo hii. Tutakuwa na wasanii wengi pamoja na wadau mbalimbali wa Musiki na pia utapata muda kupiga picha na msanii huyo na Tuzo yake.
Mtaalamu wa Ustawi wa mwajiriwa Bw. Doug Bramsem akitoa somo katika semina juu ya Ustawi wa Mwajiriwa iliyofanyika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam. Semina hiyo ilikuwa na lengo la kuwawezesha washiriki kujua nini maana ya Ustawi wa Mwajiriwa, jinsi ya kuendesha kampuni na kupata faida na kujua historia ya Ustawi wa Mwajiriwa nchini Tanzania na kumjenga mfanyakaziwako kuwa bora na kutatua ustawi wake katika kampuni zao
 Mtaalamu wa Ustawi wa mwajiriwa Bw. Doug Bramsem akikazia neno.
Washiriki wakifuatilia semina.
Mtaalamu wa magonjwa ya akili kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha magonjwa ya akili, Prof. Gad Kilonzo akizungumzia Ustawi wa Mwajiriwa.
 Mtaalamu wa mambo ya Saikolojia, Bi. Lisa Finke kutoka GIZ akitoa somo katika semina hiyo.
 Mtaalamu wa Ustawi wa mwajiriwa, Dkt. Hilde Basstanie kutoka GIN akitoa somo la ugonjwa wa Ukimwi jinsi ya kujilinda makazini.
 Washikiri wakifuatilia kwa makini semina hiyo.
Mmoja ya washiriki wa semina hiyo, Bw. James Lwanga kutoka hospitali ya Kadic iliyopo Bukoto, Uganda akielezea mambo mbali mbali yanayofanyika katika jamii nchini kwao.
 Washiriki wakifuatilia kwa makini semina.
  Mtaalamu wa Ustawi wa mwajiriwa,  Dkt. Hilde Basstanie (kwanza kulia) kutoka GIN akiwa na washiriki wengine wakifuatilia kwa makini.
Washiriki wakiwa makini kupata somo.


Umewahi kulisikia hili neno?

Kwa ufupi linasanifu dhana nzima ya AFYA.

Ila afya hii inaweza kuwa ya kimwili (physical), kiakili (mental), kipesa (financial), kinahusiano (relationship), kijamii (social), kikazi(occupational), kiroho (spiritual), kihisia (emotional), kimazingira (environmental) na hata ya kitabibu (medical).
Tunahitaji afya zote hizi kuwa kamili na wenye furaha (for optimal well-being).

Dhana hii ya WELLNESS itaelezewa kwa ufupi kwa nini ni muhimu kwako katika hotel wa Blue Pearl, Ubungo Plaza, jumapili tarehe 2 Desemba 2012 toka saa 8 mchana hadi 1 jioni. Wataalam wenye uzoefu katika fani hii watakuelimisha kwa muda mchache.
Uzinduzi huu utasindikizwa na mwanamuziki WAHU KAGWI toka Kenya akikuambia BETTER DAY. “Whatever you are going through today, there always gonna be a better day”.
Kiingilio: 20,000/= only per head

COME ONE, COME ALL.
Tickets zitapatikana 8020 fashions Sinza, maduka yote ya Mariedo ambayo ni IPS, Benjamini Mkapa Towers na Namanga , mlimani city Shear Illusions na Milepamba shop Mwenge Bus stop.
NB: HAKUNA TIKETI ZITAKAZOUZWA MLANGONI SIKU YA JUMAPILI. Deadline Jumamosi saa 4 asubuhi. Only limited seats
NB: Get ready to step on GREEN CARPET for pictures, the carpet of HEALTH

THT is offering a special package of entertainment for this festival season.

• Traditional dances
• Indian dances
• Bongo flavor artists
• Modern dances
• Contemporary dances
• Kids games and activities

Contact THT (Tanzania House Talent)
N0: +255 786 608 022

                    ‘You relax while we plan for you’
 DICKSON VEDASTUS WASIWASI ALIZALIWA 7/07/1996 KATIKA HOSPITALI YA RUFAA BUGANDO MWANZA, KIBOFU CHA MKOJO KIKIWA NJE (KIKIONEKANA WAZIWAZI), MADAKTARI WAMEMFANYIA MATIBABU KUPITIA OPARESHENI MARA TATU BILA MAFANIKIO.

OPARESHENI YA KWANZA ILIFANYIWA AKIWA NA MIEZI MIWILI, OPERESHENI YA PILI IKAFUATIA NA YA TATU IKAFANYIKA MWAKA 2000 HAPO HAPO HOSPITALI YA BUGANDO, LAKINI KWA BAHATI MBAYA ZOTE HAZIKUZAA MATUNDA.
KWA MUJIBU WA MZAZI WA KIJANA DICKSON, BW. VEDASTUS WASIWASI AMBAYE NI MKAZI WA MTAA WA SONGAMBELE, MAGOMENI KIRUMBA KATIKA  JIJINI MWANZA AMESEMA KUWA ALIPEWA USHAURI NA MADAKTARI WA HOSPITALI HIYO KUMPELEKA NCHINI INDIA KWA MATIBABU ZAIDI.


GHARAMA ZA MATIBABU NI SHILINGI MILIONI 20, NAYE HANA UWEZO HIVYO AMEOMBA WASAMALIA WEMA KUMSAIDIA KUNUSURU ADHA NA MATESO AYAPATAYO MTOTO WAKE.

 CHANGIA KUPITIA AKAUNTI ZIFUATAZO:-

CRDB     0152457709500

AZANIA 003003005102370001

SIMU 0762324527 OR 0683580004
 LEO tulipata fursa ya kuzungumza na mzazi wa mtoto anayehitaji upasuaji (Dickson) Bw. Vedastus Wasiwasi kujua usumbufu na adha aipatayo mtoto naye kwa ufupi alikuwa na haya ya kuongea.. ZAIDI NA ZAIDI TEMBELEA gsengo.blogspot.com