Washiriki wa shindano hilo wakiwa katika pozi la pamoja.
Meneja matukio wa Dar Live, Abdallah Mrisho, akielezea namna burudani zitakavyopamba za kesho ndani ya ukumbi huo.


Baadhi ya waandishi wa habari na washiriki wa shindano hilo wakisikiliza ufafanuzi wa waandaji wa mchakato huo.


Mratibu wa shindano la The Mic King, Luqman Maloto (katikati), akielezea kwa ufasaha mchakato wa kuwapata washiriki hao ulivyofanyika.
Washiriki wakisikiliza kwa makini utambulisho wao kwa wanahabari leo.

Wanahabari wakichukua matukio wakati wa utambulisho huo.

Washiriki wa shindano hilo wakiwa katika pozi la pamoja.
---
WASHRIKI wa shindano la The Mic King linaloratibiwa na uongozi wa Ukumbi wa Taifa wa Burudani wa Dar Live, leo wametambulishwa rasmi kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya hapa nchini.

Utambulisho huo umefanyika ndani ya Ukumbi wa The Atriums Hotel iliyoko Sinza-Afrika Sana jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mratibu wa Shindano hilo, Luqman Maloto, alisema amelazimika kutoa utambulisho huo leo kwa kuwa kesho washiriki hao watachujwa ndani ya Ukumbi wa Dar Live kwa mara ya kwanza tangu walipoingia kwenye

Top 20.
Maloto amewaomba mashabiki wa burudani waje kwa wingi kesho ndani ya ukumbi huo ili waweze kujipatia fursa ya kumchangua mkali katika shindano hilo ambalo fainali zake zinatarajiwa kufanyika Machi mwaka ujao.
Pia meneja matukio wa Dar Live, Abdallah Mrisho, amesema kesho katika utambulisho huo kutakuwa na shoo ya nguvu inayofahamika kwa jina la Usiku wa Wanyama, ambapo wasanii kibao mashuhuri watatumbuiza.
(Habari/Picha: Musa Mateja/GPL)
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: