MMILIKI
wa gari ambalo lilikuwa likiendeshwa na msanii maarufu nchini,
Hussein Ramadhan ‘Sharo Milionea’ na kupata nalo ajali
iliyosababisha kifo chake huko Muheza, Tanga, Mohammed Ismaili
maarufu kwa jina la Mudi Suma, ameibuka na kueleza uhusiano wake na
marehemu, huku akisema amekubali hasara.
Akizungumza
kwa simu kutoka Muheza jana Suma alisema hana mpango wa kudai fidia
au kupeleka malalamiko yoyote kwa ndugu wa marehemu kwa kuwa;
“Kilichotokea ni kazi ya Mungu.” “Siwezi kudai hata kidogo
hivyo ni vitu vya kupita tu.
Marehemu alikuwa ni zaidi ya ndugu yangu, gari ni kitu kidogo sana katika uhusiano tuliokuwa nao,” alisema Suma na kuongeza kwamba hata Marehemu Sharo Milionea naye alikuwa amemwachia mali zake kadhaa ikiwamo gari. “Siyo gari tu alilokuwa ameniachia. Kuna mikataba yake ya kazi, Bajaji yake na funguo za chumbani kwake. Nasubiri kukabidhi vitu hivyo baada ya kukaa na ndugu zake. Vitu viko kwenye mikono salama,” alisema.

Kuhusu
gari lake lililopata ajali, Suma alisema lilikuwa na bima ndogo,
lakini anapanga kwenda TRA atakaporejea Dar es Salaam kufuatilia
baadhi ya mambo.
“Kabla
ya kuondoka bima ile kubwa ilikuwa imekwisha kwa hiyo nikaamua
kuikatia bima ndogo. Nitakapofika kesho (leo) Dar es Salaam,
nategemea kwenda ofisi za bima kuzungumza nao,” alisema
Suma.
Alipoulizwa kama kuna mtu mwingine atakayeathirika
kutokana na gari hilo kuharibika katika ajali mbali na yeye, alijibu:
“Hakuna tofauti na mimi mwenyewe na familia yangu.”
Kabla ya ajali.
Suma alieleza kuwa kabla ya kuanza safiri yake, Sharo Milionea alifika nyumbani kwake mchana na kumweleza kuwa afya yake haikuwa nzuri. “Kabla ya kuondoka aliniambia kuwa hajielewi elewi na kifua kilikuwa kinambana. Nikamshauri asiondoke peke yake, atafute mtu wa kuondoka naye ambaye atamsaidia kuendesha gari njiani,” alisema Suma na kuongeza:

“Tulianza
kuwapigia simu jamaa zetu wanne wa kusafiri naye lakini kila
tuliyemwambia hakuwa tayari. Ilikuwa ni changamoto mpaka ilipofika
saa 10:45 hivi jioni, akaamua kuondoka peke yake. Wakati anatoa gari
getini kwangu, nikamwambia, basi jaribu kuwa mwangalifu sana, maana
alikuwa kweli anasumbuliwa na kifua. Tukakubaliana kwamba atakaporudi
aende hospitali kucheki afya yake.”
Kuhusu
uhusiano wake na marehemu, Suma alisema: “Mimi ni mfanyabiashara na
yeye alikuwa msanii, lakini ilitokea tukawa marafiki sana mpaka
ikafikia wakati nikaona kuwa ni ndugu yangu. Nilimwamini nikamtambua
kama sehemu ya familia.”
Alisema
marehemu alikuwa akitumia gari hilo kila alipolihitaji na safari ya
kwenda nalo Tanga kwa wazazi wake ilikuwa ni ya tatu.“Siyo mara ya
kwanza kuitumia gari lile, nilikuwa nimemwamini sana. Safari ya
kwanza alichukua na kusafiri nalo mwenyewe, halafu safari ya pili
ikafuata na hii ilikuwa safari ya tatu,” alisema Suma.
Eneo
la ajali wakimbia makazi
Baadhi ya wakazi
wa Kijiji cha Songa Kibaoni mahala ambako Sharo Milionea alipatia
ajali, wamezikimbia nyumba zao baada ya Mkuu wa Wilaya ya Muheza,
Subira Mgalu kutoa siku moja kwa waliopora mali za marehemu huyo
kuzisalimisha mara moja.
Toa Maoni Yako:
0 comments: