Meneja wa Intaneti tigo Bw. Titus Kafuma akiongea na waandshi wa habari
leo katika Hoteli ya JB Belmont jijini Dar es Salaam wakati wa
kuchezesha droo ya kwanza ya wateja wanaotumia huduma ya tigo smart card
ambayo imechezeshwa leo kwa mara ya kwanza mara ya droo hiyo kuanzishwa
rasimi mwezi septemba mwaka huu ambapo washindi 42 wamepatikana huku
washindi watatu kila mmoja amejishindia vocha ya shilingi 50,000 za
kununua bidhaa kwenye maduka ambayo tigo itawaelekeza kununua bidha hizo
huku washindi wengine wamejishindia tiketi za kuangalia mpira wengine
sinema na wengine kwenda kwenye klabu za mziki na wengine wamejishindia
tiketi kwa ajili ya mlo wa usiku katika hoteli ambayo tigo itawagaramia
kilakitu.
Afisa uhusiano wa Tigo;Bi.Tuli Mwaikenda akisisitiza jambo wakati wa droo ya Tigo smarti card leo.
Afisa
uhusiano wa Tigo Tuli Mwaikenda (katikati) na kulia Bw. Mkumbo
Myonga, kushoto ni Bw. David Sekwao wakiteta jambo wakati wa Droo ya tigo
smati card iliofanyika leo katika Hotel ya JB Belmont jijini Dar es
salaam.
David Sekwao kushoto akichezesha Droo hiyo huku akishuhudiwa na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.


Toa Maoni Yako:
0 comments: