Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar
VIONGOZI wanane wa makundi mawili ya Kiislamu Zanzibar wamefikishwa
katika Mahakama Kuu ya Vuga mjini Zanzibar wakituhumiwa na mashita
manne yanayohatarisha usalama wa taifa.
Waliofikishwa katika Mahakama hiyo ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Maimamu mjini Zanzibar Sheikhe, Faridi Hadi Ahmedi na Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Uamsho Sheikhe, Mselem Ali Mselem.
Wengine ni Mussa Juma Issa, Suleiman Juma Suleiman, Azan Khalid
Hamdan, Khamis Ali Suleiman, Hassan Bakar Suleiman na Ghalib Ahmada
Omar.
Mbele ya Mrajisi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, George Kazi Mwendesha
Mashtaka wa Serikali, Rayah Mselem alidai katika mahakama hiyo kuwa
watuhumiwa wote kwa pamoja wanatuhumiwa kati ya Oktoba 17 na 18 mwaka
huu mchana na mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar, chini ya kifungu namba
16 kifungu kidogo cha tatu(d) sura ya 47 ya sheria ya Usalama wa Taifa,
walitoa lugha ya uchochezi uliosababisha vurugu, ghasia na kuharibu mali
yakiwemo majengo na barabara.
Mwendesha mashitaka huyo pia aliendelea kudai mahakamani hapo kuwa,
kati ya Mei 26, na Oktoba 19, mwaka huu, Viongozi hao waliwahamasisha
wananchi mbalimbali wa mji wa zanzibar na viunga vyake kwa maneno ya
uchochezi na kusababisha machafuko yaliyosababisha uhalibifu mkubwa wa
mali katika maeneo mbalimbali ya mji wa zanzibar.
Rayah ameyataja maeneo ya mji wa Zanzibar yaliyoathiriwa zaidi na
machafuko hayo kuwa ni Lumumba, Msumbiji, Fuoni, Meli Sita na Mbuyuni.
Hata hivyo watuhumiwa hao hawakutakiwa kujibu lolote kutokana na
mashitaka yanayowakabili kuwa ni ya kuhatarisha usalama wa taifa.
Pamoja na watuhumiwa hao kudai na kuomba dhamana, mahakama hiyo
haikuweza kutoa dhama kutokana na Hati ya iliyowasilishwa mahakamani
hapo na Mkurugrnzi wa mashitaka wa zanzibar ya kuzuia dhamana za
watuhumiwa hao chini ya kifungu namba 19 kifungu kidogo cha (1) na cha
pili (2) sura ya 47 ya Sheria ya Usalama wa Taifa iliyofanyiwa
marekebisho mwaka 2002.
Watuhumiwa wote wamerudishwa rumande hadi Novemba 8, mwaka huu kesi yao itakapokuja tena kwa kutajwa.
Hiyo ni kesi ya pili kwa watuhumiwa saba na kesi ya kwanza kwa
mtuhumiwa hao isipokuwa kwa mtuhumiwa wa nane Ghalib Ahmed Omari ambaye
hiyo ni mara yake ya kwanza kufikishwa mahakamani.
Mtuhumiwa Galib ambaye alikuwa akitafutwa na Polisi kwa kuhusika na
makosa yaliyompeleka mahakamani, alikamatwa juzi alipoonekana kwenye
maeneo ya mahakama ya wilaya ya Mwanakwerekwe kusikiliza kezi za wenzao.
Mara walipoondoka katika ukumbi wa Mahakama kuu ya Vuga,
washitakiwa wote saba, walipelekwa katika Mahakama ya Wilaya ya
Mwanakwerekwe ambako nako jana pia walipaswa kwenda kusikiliza uwamuzi
wa au watapatiwa dhama ama vinginevyo.
Hata hivyo mahakama hiyo kesi hiyo imetajwa tu na uwamuzi wa
watuhumiwa kupewa au kutopewa dhama katika kesi hiyo ya kwanza utatolewa
Novemba 7, mwaka huu.
Watuhumiwa hao wamerudishwa rumande katika Gereza la Chuo cha Mafunzo Ziwani.
Toa Maoni Yako:
0 comments: