(Picha ya mti hapo ndipo nitakapofanyia Party yangu huo mti upo ndani ya Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni)
---
KAMPUNI ya Tigo Tanzania , October 21, Jumapili  inatarajiwa kumfanyia sherehe maalum ya siku ya kuzaliwa, mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima na mwanablogs, Andrew Chale atakayejumuika na watoto mbalimbali wakiwemo wale wanaoishi kwenye mazingira magumu ndani ya viunga vya Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na mtandao huu,  Benny Lutaba, Ofisa masoko kutoka kampuni hiyo ya mawasiliano, alisema waliendesha shindano la ‘Sheherekea na Tigo’ kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook, kwa wateja wa Tigo nchini, na Chale kufanikiwa kushinda nafasi ya pili kati ya washiriki zaidi ya 30, hivyo kubahatika kufanyiwa sherehe hiyo maalum.
“Wateja wetu wa Tigo waendelee kutuunga mkono, kwani kuna vitu vingi sana katika kusaidia jamii, ikiwemo hii ya ‘Sheherekea na Tigo’ na washindi mbalimbali wanabahatika kujumuika kwa pamoja na familia zao kusheherekea pamoja,” alisema Lutaba.
Kwa upande wake, Chale alisema kuwa, sherehe hiyo anatarajia kufurahia na watoto mbalimbali, wakiwemo wale waishio kwenye mazingira magumu kutoka vituo mbalimbali kama Mitindo House, Umra, Dogodogo Center  Kigogo na watoto wa majumbani, wakiwemo wa marafiki zake.
Aidha, Chale alisema kuwa, watoto hao watabahatika kutembelea sehemu mbalimbali ndani ya Nyumba hiyo ya Makumbusho na Utamaduni, kujifunza mengi pamoja na kupata zawadi mbalimbali kutoka kwa American Garden ambao watajumuika nao kwenye viunga hivyo vya Makumbusho.
Akizungumzia hilo, mmoja wa wawakilishi wa American Garden,Miraji Chambuso alisema kuwa  watajumuika kwa pamoja kwa kutoa vitu mvalimbali kwa watoto watakaojitokeza  kwenye sherehe hiyo maalum.

Shindano hilo lilikuwa maalum kwa ajiri ya wateja wa mtandao wa Tigo waishio jijini Dar es Salaam, ambako walikuwa wakihitajika washindi sita.
Aidha, Chale alitumia wasaha huo kwa ndugu na jamaa kuwa na mazoea ya kuwajali watoto waishio kwenye mazingira magumu na hatarishi kwa kuwatembelea kwenye vituo na kuwapatia misaada ama kuwajulia hali.

"Kwa kuwaalika watoto hawa, ni kuhamasisha watanzania kupendelea kutembelea utalii wa ndani na hii ni stahili ya pekee kwa watanzania wengine kwani kukumbuka siku ya kuzaliwa unaweza kufanya mambo mengi  kwa jamii ikiwemo hii ya kuwatoa out watoto hasa sehemu kama hizi na kufurahia nao" alisema Chale 

Pia aliwaomba marafiki kwa mwanae atakaetaka kujumuika nae awasiliane nae kupitia +255719076376 au +255767076376 ama kama unachochote cha kuchangia.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: