Warembo wanaowania taji la Redd’s Miss Temeke 2012 wakiwa mazoezini jana kwenye Club ya TCC Chang’ombe jana. Shindano hilo litafanyika Ijumaa hii Sept 21, kwenye ukumbi wa PTA (Sabasaba Hall). (Picha na Intellectuals Communications Limited).
---
Na mwandishi Wetu.
Kamati ya Redds Miss Tanzania leo imewambelea kambi ya Redd’s Temeke 2012, kubwa ni kuwafunda vimwana hao kutoka Vitongoji vya Kigamboni, Kurasini na Chang’ombe, kuhusu mambo mbalimbali ndani ya mashindano yea urembo.
Kamati hiyo iliongozwa na Mkurugenzi wake, Hashim Lundenga aliyefuatana na mshauri wa masuala ya urembo katika kamati yao, Dk. Ramesh Shah, katibu Bosco Majaliwa, Mkuu wa Itifaki, Albert Makoye na mjumbe wa kamati hiyo, Lucas Rutta.
Shindano la Redd’s Miss Temeke, linatarajia kufanyika Ijumaa hii katika ukumbi wa PTA (SabaSaba Hall) na tiketi za VIP zimeshaanza kuuzwa katika Club za City Sports Lounge iliyopo makutano ya Samora na Azikiwe na Nyumbani Lounge iliyopo maeneo ya Namanga ambapo VIP kwa mtu mmoja ni Tshs 50,000 na pia waweza nunua kwa meza moja ama ya watu 8 kwa laki 4 au watu kumi laki 5.
Warembo wanaowania taji hilo ni Agness Goodluck, Angela Gasper, Flaviana Maeda,Edna Sylvester, Catherine Masumbigana, Khadija Kombo, Neema Doreen, Flora Kazungu, Lilian Joseph, Elizabeth Peter, Elizabeth Boniphace, Jesca Haule, Zulfa Bundala, Mariam Ntakisivya na Esther Albert.
Shindano hili litakuwa ni miongoni mwa mashindano ya lala salama kabla ya kupata warembo watakaoungana na warembo wa kanda nyingine kuingia kambini kumtafuta mrembo wa Redds Miss Tanzania kwa Mwaka huu.




Toa Maoni Yako:
0 comments: