Waandishi wa Habari wakiwa wamebeba Mwili wa Marehemu kuelekea Makabirini
Wakiwa wanafanya ibada ya Mwisho kabla ya kuanza maziko
Hapa wakiwa wanashusha mwili wa marehemu katika Nyumba yake ya milele
Mwili wa Marehemu Daudi Mwangosi ukiwa tayari katika kaburi.
 Mke wa Marehemu Daudi Mwangosi akiweka Shada la Mauwa kwa machungu
 Mke wa Daudi Mwangosi akiwa analia kwa uchungu katika Kaburi la Marehemu Mumewe.
 Watoto wa Marehemu wakiwawanaweka mashada ya maua sasa.
 Dr Slaa akiweka Shada la maua.
Dr. Slaa baada ya kumaliza kutoa heshima za mwisho
Mh. Mark Mwandosya akiweka taji la maua pamoja na mke wake 
 Rais wa UTPC akiweka shada la Maua.
Mwenyekiti wa Mbeya Press Club akiweka shada la maua 
Mwandishi Mkuu wa Mbeya  yetu Blog, ndugu Joseph Mwaisango akiwa anatoa heshima zake za mwisho katika kaburi.
Wananchi wakiwa wanarejea baada ya mazishi.
Na huu ndio mwisho wa tukio zima la mazishi ya marehemu, Mpiganaji Daudi Mwangosi aliyekuwa mwandishi wa Television ya Chanel 10. 
PICHA KWA HISANI YA MBEYA YETU BLOG.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

1 comments:

  1. Mie nasikitishwa sana na tabia ya raia wenzangu ya kushindana na vyombo vyetu vya dola anayoendelea kushika kasi nchini. Matokeo yake ni kupoteza maisha ya vijana wetu wabichi kabisa tena wengi wao wasiohusika na vurugu zenyewe! Chonde chonde watanzania, tutii sheria, maelekezo na amri halali za vyombo vya dola. Tutoe ushirikiano wa ulinzi na usalama. Ukiwekwa chini ya ulinzi tii. Mwisho wa siku ukweli utadhihiri utakuwa huru. Hakuna chombo cha dola kinachokusudia kumwonea mtu wala kumnyanyasa. Natoa pole sana kwa familia za misiba yote yote miwili yaani ule wa iringa na morogoro. Naomba jamii iamini kwamba polisi yetu ya tanzania haikukusudia yaliyotokea kutokea. Kwa maoni yangu, yaliyotokea ni ni kutokana na mazingira magumu wanayokutana nayo ktk utekelezaji wamajukumu yao ya ulinzi na usalama. Unajua ktk hali ya kawaida polisi anapoamru jambo halafu raia anapinga kwa kweli inampa wakati mgumu sana askari. Watanzania tuwaepuke wavurugaji wa amani na wachochezi wa kuvunja amani.

    ReplyDelete