Padre Kalaso (kati) wa Kanisa la Familia Takatifu Parokia ya Ipuli, Tabora akishuhudia Bwana Allen Munene akimvalisha pete bibi Veronica Stima wakati wakifunga ndoa takatifu iliyofanyika kanisani hapo na kufuatiwa na sherehe katika ukumbi wa chuo cha Utumishi wa Umma Uhazili, Tabora.
Bibi Veronica Stima akimvalisha mumewe Allen.
Wakiwa katika nyuso za tabasamu zito ni Bwana na Bibi Allen Munene.
Padre Kalaso (kati) wa Kanisa la Familia Takatifu Parokia ya Ipuli, Tabora akimuelekeza Bwana Allen Munene kutia saini katika cheti huku pembeni yake mkewe Veronica akishudia.
Nae mkewe akitia saini.
Wakiwa katika nyuso za furaha na kuonyesha vyeti vyao.
Pongezi nyingi zikiwamiminikia Bwana na Bibi Allen mara baada ya kufunga pingu za maisha.
Mama mzazi wa Bibi harusi akitoa baraka zake za pekee kwa mwanae mpya wa kiume ambaye ameungana na mwanae.
Pozi la pekee; bibi harusi akiwa na wasimamizi wake.
 ...Maharusi wakiingia ukumbini kwa furaha.
 
...wakishangiliwa mara baada ya kukata utepe na kuingia ukumbi.
...wapambe nao wakiingia kwa madaha.
Bibi Veronica akigawa shampeni kwa wakwe zake.
 Nae bwana Allen Munene akigawa shampeni upande wa wakwe zake.
 ...Tunywe kwa afya na maisha yetu...
Wapendanao wakikata keki kuonyesha umoja na upendo kati yao.
 Maharusi wakigawa keki upande wa Mzee Munene. Ikiwa ni ishara ya kuwashukuru wazazi kwa mambo waliyowafanyia.
 ...Huku nako Baba na Mama Stima wakipokea keki ya shukrani kutoka kwa watoto wao.
 ...nderemo na vifijo vilitawala ukumbini...
 Wachanga na ile staili yao ya kushikana mikono, kudumisha umoja na mshikamano kati yao.
 ... Upendo na mshikamano udumu milele.
 Wapare nao hawakuwa nyuma na staili yao ile ya kuwema mikono nyuma...
 Wafipa sasa wao walikuja kisasa kabisa...
Mama mzaa chema akiserebuka kwa raha zake.
 ...huku nako mambo ya pwani yaliendelea kunoga...
 ... Ni bwana Cathbert Angelo (kati) mmiliki wa mtandao huu, nikiwa na mama na baba (wakwe zangu).
 Maharusi wakiondoka ukumbini kwa mwendo wa madaha.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

1 comments:

  1. Harusi hii ilikuwa safi sana...mliipanga ikapangika... mmependeza kusema kweli..

    Hongereni sana.

    ReplyDelete