AJALI nyingi za barabarani nchini husababishwa na madereva wazembe wasio zingatia
sheria za matumizi sahihi ya barabara. Miongoni mwa ajali hizo nyingi husababishwa na madereva hao kuovatake magari mengine katika kona au milima kama basi hili linavyofanya katika kona ya Lugalo mkoani Iringa. Madereva “PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA”.
Basi hili linguine nalo lilikuwa linafanya makosa hay ohayo ya kulipita gari lingine katika miinuka na kona kali za mlima Kitonga.
Polisi wa Kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Iringa, akiwepo RTO, SP. Pamphil Honono (kushoto) walimuona na kumsimamisha dereva wa basi hilo. Matukio haya yanatokea ndani ya wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa. 
Dereva huyo alikuwa ni Issack Gerald Nyamaiswe Mkazi wa Mjini Dodoma.   
Nahapa Askari wa Kikosi cha Usalama barabarani akimwandikia Notfication dereva huyo. 
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: