Wananfunzi wa Shule ya Msingi Mbezi ya Jijini Dar es Salaam, nao hawakuwa nyuma katika kudai haki yao ambapo nao walifikisha ujumbe kwa njia hii ya Bango, wakiwa pembezoni mwa barabara Morogoro Jumatatu ya tarehe 30.8.2012 asubuhi.
---
Hivi majuzi nilishtushwa sana baada ya kusikia kuwa nao walimu wameamua kufanya migomo ili kuitaka serikali iwalipe madai yao, niliogopa sana na kuanza kujiuliza ni kitu gani kimetokea mpaka nchi yetu ya Tanzania sasa imekuwa ni ya maandamano na migomo ya kila kukicha???.


Hali kadharika nilizidi kupata mshangao pale niliona wanafunzi wa shule za msingi nao wameamua kufanya maandamano kuwapinga walimu wao ambao waliamua kufanya mgomo ili kuishinikiza serikali iwalipe madai yao.

Jambo la kujiuliza mwanamchi mwenzangu ni nani aliyewapa ujasiri watoto hawa mpaka wakaandika mabango na kuamua kuandamana??? Ni vyema wazazi pamoja serikali wakawa macho kwa vile Taifa lisilo na misingi si taifa jema??? Tunapoelekea kwa sasa umefika wakati viongozi kuacha kufumbia macho madai ya watu.

Sishangai kuona vijana hawa wakiwa wakubwa wakafika hatua ya chuo kikuu kuendelea na migomo; ni vyema tukaanza kukunja makucha yao ingali bado wadogo ili baadae wasije kuleta madhara makubwa katika jamii maana wahenga walisema, "Samaki Mkunje Angali Mbichi".

Pia ningewaomba wazazi kuacha kufumbia macho haya ambayo yanatokea sasa maana hali hii ni hatari sana katika familia na taifa letu kwa ujumla.

Vile vile viongozi wa nchi na watawala wote wakajiuliza ni kidudu gani kimeikumba nchi ya Tanzania ama imebaki kuwa ni hadithi za hapa na pale, nitadiliki kusema kuwa, "MFICHA MARADHI KIFO HUMUUMBUA"
 
Maana kwa sasa nimesikia msemo usemao, "TANZANIA BILA MIGOMO HAIWEZEKANI", watu wamechoshwa na ahadi hewa za kila siku.

Ujumbe huu umeletwa kwenu;
 Cathbert Angelo Kajuna
 Mmiliki wa Kajunason Blog.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: