Na Mohammed Mhina wa Jeshi la Polisi –Zanzibar

Zoezi la kuitafuta Meli ya MV Skagit linalofanywa na Wazamiaji wa Majeshi na Vikosi vya Ulinzi na Usalama Zanzibar, limezidi kuwa gumu baada ya wataalamu hao kushindwa kuiona meli hata baada ya kuzamia na kuisaka meli hiyo katika eneo ilipozama meli hiyo.

Meli hiyo ambayo ilipinduka na kuzama katika eneo la kisiwa cha Chumbe umbali wa 14 Notcomail vipimo vya majini, haijaonekana tena tangu siku ya tukio.

Wakizungumza baada ya kusitisha zoezi hilo, Wazamiaji hao wamesema wamelazimika kuzamia chini ya bahari na kufanya uchunguzi katika eneo la upana wa zaidi ya kilometa moja bila ya kuiona meli hiyo.
 
Washiriki wa zoezi hilo kutoka Jeshi la wananchi, Polisi, KMKM, Mamlaka ya Bandari Zanzibar pamoja na makampuni ya watu binafsi katika utafutaji wa meli hiyo kurudi mikono mitupu kwa sababu ya uhaba wa vifaa.

Wakizungumza katika eneo tukio baadhi ya wazamiaji hao wamesema kuna uwezekano kuwa meli hiyo imekokotwa na maji katika kina hicho cha bahari.
 
Wamesema kuwa ili zoezi hilo lifanikiwe ni lazima vipatikane vifaa maalumu vitakavyosaidia kuchunguza mali ilipo meli hiyo kabla ya wazamiaji hawajafikaa katika eneo hilo.

“Meli hiyo imeshindikana kuonekana kutokana na ukosefu wa vifaa vya kusaidia ugunduzi wa mahali ilipo meli hiyo”.

Alisema Bw. Ali Ramadhani, kutoka Kampuni ya Easy Blue Divers. Amevitaja baadhi ya vifaa hivyo kuwa ni Fish Finder na Eco Sounder pamoja na Soner Ditector.

Naye Bw. Issa Juma Mohammed, wa Kampuni ya Azam Marine, amesema kuwa wao wana uwezo wa kuzamia kina cha urefu wa mita zaidi ya 50 chini ya bahari na vikiwemo vifaa hivyo vitawawezesha kubaini eneo ilipo meli hiyo kabla ya wao kuanza uzamiaji.

Zoezi la kuitafuta meli hiyo lilianza jana (juzi) kwa lengo la kutafuta miili zaidi ya watu waliozama pamoja na meli hiyo baada ya maili zilizokuwa zikiielea kutoonekana tena.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: