Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi- Zanzibar

ZAIDI ya wafuasi  40 wa kikundi cha Jumuiya ya Uamsho Zanzibr wamekamatwa na Polisi kufuatia vurugu zilizotokea jana  kwenye eneo la Darajani mjini Zanzibar.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar ACP Aziz Juma Mohammed, amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa baada ya kufunga barabara kadhaa kwa mawe, vyuma, matofari na kuchoma moto matairi ya magari.

Kamanda Aziz amesema kuwa katika vuurugu hizo hakuna Askari ama watuasi wa kikundi hicho waliofariki ama kujeruhiwa wakati wa ghasia hizo zilizokuwa nimeendelea katika mitaa mbalimbali ya mji wa Zanzibar.

Amesema wafuasi hao walitumia mawe, chupa  na vipande vya mbao kuwarushia Polisi lakini amesema hadi kumalizika kwa zoezi la kuwatawanya wafuasi hao saa nane usiku wa kuamkia leo, (jana). 

Hata hivyo Kamanda Aziz amesema bado Jeshi la Polisi linaendelea kuwasaka viongozi wa kikundi hicho ambao wametoroka mara baada ya kuibuka kwa vurugu hizo.
Amesema vurugu hizo ambazo zilianza jana majira ya saa 11.00 jioni, zilidumu hadi saa 8.00 usiku kufuatia wafuasi wa kikundi hicho kujikusanya katika maeneo mbalimbali wakifanya vurugu.

“Tunawatafuta viongozi wa kikundi hicho na tunawataka popote walipo wajitokeze na kujisalimisha wenyewe Polisi.” Alisema Kamanda Aziz.

Mara baada ya kuanza kwa ghasia hizo na hadi asubuhi ya leo (jana) barabara za Darajani na mlandege, mitaa iliyokuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu, ilikuwa haia hata mtu mmoja na hata biashara zilisimama.

Hata hivyo biashara mbalimbali zimerudia tena katika hali yake ya kawaida huku watumishi wa Baraza la Manispaa ya mji wakiendelea na kazi ya uongoaji wa mawe, matofari na mabaki ya majivu ya matairi ya magari.

Ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa Polisi endapo watawaona ama kubaini mahala walipojificha viongozi wa kundi hilo la uamsho ili wahojiwe kwa tuhuma za kuanzisha ghasia.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: