Wachezaji wa timu ya mashabiki wa timu ya Manchester City ya Uingereza wakichuana vikali na mchezaji wa timu ya mashabiki wa timu ya Real Madrid huku wakati wa tamasha la mashabiki wa vilabu vya Ulaya linalojulikana kama Serengeti Fiesta Soccer Bonanza, ambalo linafanyika jijini Mbeya katika viwanja vya Chuo cha Uhasibu (TIA) na kushirikisha timu za mashabiki wa vilabu vya Manchester United, Liver Pool, Bayern Munichen, Asernal, Manchester City Barcelona, Chealsea na Real Madrid, Mshindi katika bonaza hilo atajishindia shilingi 500,000.
Wachezaji wa timu ya mashabiki wa Barcelona wakichuana vikali na wachezaji wa timu ya mashabiki wa Chealsea katika bonanza hili timu hizo ndiyo zilizofungua dimba.
Mratibu wa Serengeti Fiesta Soccer Bonanza Shafii Dauda akitoa maelekeza kwa timu za mashabiki wa Chealsea na Barcelona kabla ya kuanza kwa mtanange wao.
Timu ya mashabiki wa Manchester Unitedi wakishangilia wakati wimbo wao ulipokuwa ukipigwa.
Timu ya Mashabiki wa Chealsea nao wakiimba wimbo wao kabla ya kuanza kwa bonanza hilo.
Timu ya mashabiki wa Arsenal wakiimba wimbo wao huku wakishagilia.
Nao Barcelona hawakuwa nyuma wakirukaruka kwa furaha mara baada ya kupigiwa wimbo wao.
Hawa ni Real Madrid kama unavyowaona katika picha wakishangilia na kucheza wakati wimbo wao ukipigwa.
LiverPoool wakishangilia kwa nguvu wimbo wao.
Mwamuzi wa mchezo huo akitoa maelekezo kwa timu za Chealsea na Barcelona kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Timu zote zikiwa zimejipanga tayari kwa kupigiwa nyimbo zao kabla ya kuanza kwa bonanza hilo kwenye viwanja vya TIA Mbeya.
Peter Kabaisa mmoja wa wafanyakazi akigawa jezi za kuchezea kwa makapteni wa timu hizo.
Mshauri nasaha wa masuala ya ukimwi Flora George  akitoa elimu kwa maadhi ya mashabiki waliofika katika banda la KIHUMBE
Mmoja wa watangazaji wa Clouds mwenye maneno mengi na vituko Mbwiga wa Mbwiguke ambaye ni shabiki wa timu ya Liver Pool akitoa tambo zake kwa vituko na kuvuta mashabiki wengi kumsikiliza katika bonanza hilo.
Timu ya Bayern Munichen ikishagilia kwa nguvu kufurahia wimbo wao katika bonanza hilo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: