Meneja Mauzo wa Airtel Kanda ya Pwani, Amina Keita (kushoto) akitoa zawadi ya simu kwa mmoja wa wakazi wa Mtwara, Nasra Salehe wakati wa uzinduzi wa huduma ya Supa 5 ya Airtel katika Uwanja wa Mashujaa mjini Mtwara jana. Tukio hilo liliambatana na burudani kutoka kwa wasanii chipukizi wa mkoani humo na baadhi ya wasanii maarufu kutoka katika Jiji la Dar es Salaam ambako waliohudhuria walielezwa jinsi ya kujiunga na faida mbalimbali zinazopatikana katika huduma ya Supa 5.
Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde akihutubia wakati akizindua huduma ya Supa 5 ya Airtel katika Uwanja wa Mashujaa Mkoani Mtwara jana.
Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde akihutubia wakati akizindua huduma ya Supa 5 ya Airtel katika Uwanja wa Mashujaa Mkoani Mtwara jana.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka THT, Mwansiti Almasi akikonga nyoyo za wakazi wa Mtwara waliohudhuria uzinduzi wa huduma ya Supa 5 ya Airtel katika Uwanja wa Mashujaa Mkoani Mtwara jana.
Msanii mkali wa miondoko ya bongo flava, Juma Kassim Nature 'Sir Nature' kutoka kundi la Wanaume Halisi, akifanya vitu vyake wakati wa uzinduzi wa huduma ya Supa 5 ya Airtel katika Uwanja wa Mashujaa Mkoani Mtwara jana.
Mwanamuziki wa miondoko ya hip hop, Ibrahim Mussa anayekwenda kwa jina la 'Roma Mkatoliki' akighani moja ya shairi la wimbo wake uliompatia umaarufu wa 'Pastor' katika uzinduzi wa huduma ya Supa 5 ya Airtel katika Uwanja wa Mashujaa Mkoani Mtwara jana.
Toa Maoni Yako:
0 comments: