WATUMIA BAJAJ
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, waumini hao, wakiwa wamevaa kanzu huku wakitembea na bakora mkononi walichukua jukumu la kukodi Bajaj na kuzunguka maeneo mbalimbali jijini inapofanyika biashara hiyo haramu ya ukahaba.
BARABARA YA SHEKILANGO
Vijana hao waliolenga kukomesha biashara hiyo hasa kipindi hiki cha mfungo walianzia kwenye Barabara ya Shekilango inayokatiza kwenye viunga vya Sinza, Dar ambapo kila kituo cha daladala kuanzia Afrika Sana hadi kwenye mataa ya Shekilango waliwakuta machangu na kuwatandika viboko kabla ya kutua mitaa ya Mwenge.
KINONDONI
Baada ya kufagiafagia Sinza kwa kuwaadabisha wanawake hao ndipo zoezi likahamia mitaa ya Kinondoni ambapo nao walipokea bakora za kutosha huku wengine wakitoka nduki.

KISA KUHARIBIWA SWAUMU 
Kwa mujibu wa vijana hao, walifikia hatua ya kufanya zoezi hilo baada ya muumini mmoja wa kiume kukatiza maeneo ya Corner Bar, Afrika Sana na kuvutwa kisha kuchezewa nyeti na makahaba na kusabisha kuharibika kwa swaumu yake.
Ilielezwa kuwa baada ya kukutwa na kimbembe hicho, ilibidi muumini huyo kukatiza safari yake ya kwenda kuswali msikikini mishale ya saa 2:00 usiku.

Ilisemekana kuwa aliporudi nyumbani alitawadha na kufunga safari nyingine ya msikitini na alipofika kwenye nyumba hiyo ya ibada ndipo akawasimulia waumini wenzake ambao nao walikasirishwa na kitendo hicho hivyo wakapanga kuvamia maeneo yote ya biashara hiyo ili kuwashikisha adabu.
Waandishi wetu, wakiwa kwenye mishemishe zao za kutafuta habari mishale ya saa 5 usiku waliwashuhudia waumini hao wapatao saba wakishuka kwenye Bajaj nyeusi maeneo ya Sinza wakiwa na bakora mikononi kisha kuwavaa machangu hao na kuwatandika.
Wakati wakitekeleza zoezi hilo, jamaa hao walisikia wakiwaambia: “Sisi tupo kwenye swaumu nyiye mnatutega, ala!”
HAWAHESHIMU MWEZI MTUKUFU?
Waumini hao waliongeza kuwa makahaba hao wamekuwa hawaheshimu mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan ndiyo maana wanaendeleza biashara yao hiyo ya aibu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

1 comments:

  1. Inamaana tuko chini ya Sharia?
    Hili la kulazimisha kila mtu aheshimu mwezi linatoka wapi?...ukifunga katikati ya vishawishi na majaribu ya offa za vyakula,na vishawishi vya ngono huo utakua mfungo...ukifunga unataka vishawishi vyoote visiwepo? hamia pluto!!

    ReplyDelete