Mkurugenzi wa Alliance One Tanzania Ltd Bw. Mark Mason
Kampuni ya Alliance One kwa kutumia kamati yake ya kuratibu miradi ya maendeleo ya jamii (CDPC) imeidhinisha shilingi 18,776,000 kwa ajili ya miradi mbali mbali ya maendeleo ya jamii katika kikao chake cha 13 kilicho kaa Mororgoro hivi karibuni.

Kamati ya kuratibu miradi ya maendeleo ya jamii (CDPC)  iliyoteuliwa na uongozi wa kampuni hupokea, huidhinisha na husimamia miradi yamaendeleo ya kijamii katika maeneo yanayo lima tumbaku. Kamati hii inayoongozwa na sera za kampuni kuwajibika kwa jamii inayowazunguka imejikita zaidi kusaidia miradiyaElimu, Afya na Hifadhi ya mazingira. 

Misaada inayoidhinishwa hulenga zaidi miradi iliyokwisha anzishwa na jamii lakini inamatatizo yakuendelea. Kampuni imeidhinisha msaada wa shilingi million nne laki tisa na hamsini kwa ununuzi wa vifaa vya ujenzi vya kuezeka na kuplasta jengo la dispensary huko Manyoni katika kijiji cha Mitundu; pia kununua vifaa vy ujenzi kwa ajili ya kukarabati vyumba vinne vya madarasakatika shule ya msingi ya Igombe wilayani Tabora vyenye thamani ya shilingi million nne laki sita na themanini ambapo shule ya msingi ya Limbula wilayani Urambo imepewa msaada wa shilling milioni mbili laki nne na tisini kwa ajili ya kuezeka madarasa mawili.

Maeneo mengine yaliyonufaidika na misaada hiyo ni pamoja na Kukarabati madarasa mawili ya masomo kwanjia ya kompyuta (e-learning classrooms) kwa shilingi million mbili laki mbili na themanini katika Shule ya Sekondari ya Nelson Mandela iliyopo Morogoro, Madawati 44 kwa shule ya msingi ya Pemba yenye thamani ya shilingi milioni mbili laki moja na themanini na nane na madawati 44 kwa shule ya sekondari ya Karota mbezoteza wilayani Tarime.

Misaada hii iliyoombwa na jamii kutoka wilaya zinazo lima tumbaku itafikishwa kwa wahusika mwezi Juni 2012. Akizungumzia misaada hii, mwenyekiti wa kamati ya kuratibu misaada yaki jamii ambaye pia nimkurugenzi mkuu wa kampuni, bwana Mark Mason alikaririwa akisema “Alliance One inaridhika na ushirikiano mkubwa unaotolewa na Serekali katika sekta ya tumbaku Tanzania. Tunaamini kuwa tuna wajibu wa kusaidia kupunguza umaskini kwa kujikita kwenye miradi yaElimu, Afya naMazingira. Ni imani yangu kwamba misaada hii tunayoelekeza kwa jamii ya tumbaku itasaidia kuongeza kasi inayofanywa na serekali katika kutoa huduma kwa wananchi wake.”
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: