Mmoja wa Waratibu wa maandalizi ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012 (pili kulia) Sebastian Maganga  akifafanua baadhi mambo mbele ya wageni waalikwa wakiwamo wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakati wa uzinduzi rasmi wa tamasha hilo uliofanyika kwenye viwanja vya Lidaz Club, Kinodoni jijini Dar leo, tamasha hilo linatarajia kutimua vumbi zake hivi karibuni katika mikoa mbalimbali, ambapo katika tamasha hilo mdhamini mkuu ni kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bia yake Serengeti Premium Lager, Kampuni ya mafuta ya Gapco pamoja na Push Mobile. Kauli mbiu ya tamasha hilo ni "MUONEKANO MPYA-BURUDANI ILELE-BAAAS"!
Sehemu ya zawadi mbalimbali zitakazotolewa kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,ikiwemo Magari aina ya Toyota Vitz kila moja yenye thamani ya shilingi milioni nane,Piki piki a.k.a Boda Boda 14 kila moja ikiwa na thamani ya shilingi milioni moja na nus na zawadi nyingine zikiwemo simu aina ya blackberry,Nokia.
Baadhi ya Wadau mbalimbali wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012 wakishuhudia uzinduzi huo uliofanyika kwenye viwanja vya lidaz Club,jijini dar.
Mmoja wa waratibu wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012,Sebastian Maganga akifafanua  jambo kwa umakini na kuweka  misisitizo kwa Wanahabari waliofika kwenye uzinduzi wa  tamasha hilo.
Sebastian Maganga kutoka Clouds Media Group akiwatambulisha Wadhamini wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012,Kutoka kulia ni Mkuu wa Masoko wa kampuni ya mafuta ya Gapco,Ben Temu,Meneja wa kinywaji cha Serengeti kutoka SBL,Allan Chonjo pamoja na muwakilishi wa kampuni ya Push Mobile,Bw.Rodney
Meneja wa bia ya Serengeti kutoka kampuni ya SBL,ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha la Fiesta 2012,Allan Chonjo akizungumza machache mbele ya wageni waalikwa wakiwemo wanahabari kutoka vyombo  mbalimbali,uliofanyika leo kwenye viwanja vya Lidaz Club,jijin Dar.
Bw. Rodney ambaye ni muwakilishi wa kampuni ya Push Mobile akionesha moja ya namba zitakazotumika kutoa taarifa mbalimbali za tamasha hilo litakaloanza kutimua vumbi zake kuanzia hapo kesho katika mikoa ya Arusha na Mbeya na baadaye mikoa mingine.
Pichani shoto ni Meneja mahusiano ya ndani ya kampuni ya bia ya Serengeti, Bw. Iman Lwinga akiwa sambamba na baadhi ya wanahabari waliofika kwenye uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Wageni waalikwa wakiwemo wasanii kadhaa bia walifika kushudia tukio hilo kubwa la kihistoria katiak tasnia ya burudani hapa nchini.
 Wakifuatilia kwa umakini zaidi.
Kwa mshangao mkubwa wakishuhudia uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya viwanja vya Lidaz Club.
 Wadau wakifuatilia uzinduzi huo,akiwemo Shaffih Dauda mzee wa sports bar.
 Meneja wa vinywaji vikali wa SBL, Bw. Emillian Rwejuna akizungumza na Meneja wea kinywaji cha Serengeti Premium Lager, Allan Chonjo wakati wa uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
 Mtangazaji wa Clouds FM, Millard Ayo akifanya mahojiano mafupi na msanii wa muziki wa kizazi kipya, Mwasiti kuhusiana na tamasha la fiesta kwa ujumla.
Wadadazi nao walikuwepo kunogesha uzinduzi huo wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: