Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishana Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Bw, Zelothe Stephen, Kulia akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi kuhusu Vifo vya wahamiaji Haramu Raia wa Ethiopia, Kushoto akisikiliza ni Mkuu wa polisi Wilaya ya Kongwa Bw. Davis Nyanda.
---
Na Luppy Kung’alo wa Jeshi la Polisi Dodoma

Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limewakamata wahamiaji haramu Themanini na Mbili (82) wote wanaume wenye  asili ya Ethiopia jana  majira ya 08:OOHRS asubuhi baada ya kuonekana wakitanga tanga katika vijijji vya  Chitego na Mkoka Tarafa ya ZOISA Wilayani  Kongwa mjini hapa.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma. Bw. Zelothe Stephen kuhusu vifo  vya Wahamiaji Haramu arobaini na tatu (43) vilivyotokea jana mjini humo alisema Raia hao wote wanatoka  Kanda ya Kusini nchini Ethiopia kwenye vijiji vya Kambata, Hadia na Sirite.

Alisema Kukamatwa watu hao walioingia nchini bila kibali kupitia mpaka wa Tanznia na Kenya wakielekea nchini Malawi kulifanikwa baada ya wananchi wema kuwaona na kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ambapo walifika na kufanya Operesheni Maalum ya Kuwasaka na kuwakamata.

”Wananchi kutoka vijiji hivyo ambavyo vipo umbali wa kilometa 141 toka Dodoma mjini waliweza kuona maiti nyingi zimetupwa kando ya barabara ya Kiteto – Dodoma  na baadaye kuwaona watu wengine walio hai katika harakati za kupita Porini kuelekea kijiji cha Izava Wilayani Chamwino hivyo kuingiwa na hofu na kutoa taarifa hizo.”aliongeza Kamanda Zelothe.

Alisema baada ya kupata Taarifa hizo, Jeshi la  Polisi lilifika katika eneo hilo ambako walishirikiana na wananchi wa eneo hilo, hadi kufikia jioni hiyo walifanikiwa kuwakamata  raia hao wa Ethiopia wapatao 82  ambao walikuwa wakizungumza  lugha ya kiingereza cha kubabaisha.


Kamanda Zelothe Stephen alisema kwa mujibu ya maelezo ya raia hao walisema kwamba walianza safari yao takribani miezi mitano iliyopita wakitokea Ethiopia kuelekea nchini Malawi, kupitia nchini Kenya ambako walidai kuwa ndiko kituo kikubwa cha wao kukusanywa na kuanza safari ya pamoja.

”Walipofika Arusha walitawanywa katika vikundi vidogo na kuhifadhiwa kwenye nyumba mbalimbali huku wakipewa chakula kidogo na maji na kwamba siku ambayo hawakumbuki walikusanywa usiku na kupakiwa kwenye lori moja lililofunikwa kote na kuanza safari kuelekea Malawi.” alisistiza Bw. Zelothe

Aidha Mkuu huyo wa Polisi Mkoani Dodoma alisema kuwa raia hao wakiwa njiani  baadhi yao walianza kuzirai na kufariki, hivyo walifanya jitihada za kupiga kelele na kumgongea dereva lakini hakuwa tayari kusimama hadi walipokuja kutelekezwa usiku wa manane kwenye eneo la tukio hilo na lori hilo kutoweka.

Akizungumzia Hali za maiti katika eneo zilipotupwa, alisema  maiti nyingi  zilionekana zikiwa tayari zimeanza kuharibika ambapo jumla ya  maiti (22 ) zilisafirishwa kwenda kuhifadhiwa katika Hospitali ya Serikali ya Mkoa wa Morogoro na nyingine (21) zimehifadhiwa kwenye Hospitali ya Serikali Mkoa wa  Dodoma kusubiri uchughuzi wa Daktari na taratibu.

Wakati huo huo Kamanda Zelothe amesema  huduma za kibinadamu zimekuwa zikitolewa kwa  raia hao wa kigeni, na  mahali waipohifadhiwa ni jirani na kituo cha Polisi Kati Mkoani Dodoma kwa ushirikiano na taasisi nyingine ikiwa ni pamoja na Idara ya Afya, Red Cross, Uhamiaji na Uongozi wa Mkoa.

Kamanda Zelothe Stephen aliwashukuru wananchi wa Vijiji vya Chitego na Mkoka  kwa kutekeleza zana ya Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi kwa kutoa taarifa za tukio hilo, aidha wito kwa wananchi wote kuendelea kutoa taarifa za matukio mbalimbali wasiyoyaelewa katika kamati za Ulinzi na Usalama katika ngazi za Kijiji, Kata, Tarafa. Wilaya na Serikali Kuu ili kuweza kudhibiti uhalifu katika maeneo yetu.

MAJINA YA RAIA WALIOPATIKANA WAKIWA HAI NI KAMA IFUATAVYO:-

1.    TAGASA S/O DETAMO, 24 YRS
2.    TAREKENYI S/O AMADO, 22 YRS
3.    ABELA S/O KEMISO, 20 YRS
4.    TAREKENYI S/O LINTISU, 29 YRS
5.    ZOUDE S/O TAFASA, 25 YRS
6.    HELEBO S/O BALANGO, 24 YRS
7.    MANEBO S/O MALNAMO, 20 YRS
8.    ABALAA S/O MAMUSAA, 25 YRS
9.    BILAMO S/O DEMISO, 25 YRS
10. DASTA S/O BALIGICHO, 30 YRS
11. TEKELA S/O MARKUS, 20 YRS
12. DMBALO S/O MALASA, 22 YRS
13. ADENA S/O FAYISE, 28 YRS
14. TESHUMA S/O BAIANE, 22 YRS
15. DEGEFE S/O SHIRE, 26 YRS
16. TEFERE S/O JIKAMO, 29 YRS
17. HAFTAM S/O MATWOSI, 22 YRS
18. DEJENE S/O TADESI, 21 YRS
19. DEREJE S/O SEMUEL, 20 YRS
20. TAKATAL S/O SOLOMON, 23 YRS
21.  ABEBE S/O MANEBO, 30 YRS
22. DESALGN S/O MORORO, 35 YRS
23. TAGESE S/O BAKALA, 25 YRS
24. DESLIGN S/O DANTO, 28 YRS
25. SALAMO D/O HAILE, 25 YRS
26. CHEFUMU S/O YOSEPH, 20 YRS
27. BEKELE S/O YOHANES, 23 YRS

28. SULTAN S/O ALGANO, 21 YRS
29. DEREJA S/O GILMAHIZI, 21 YRS
30. ZEKARIAS S/O SIKILO, 24 YRS
31. TEMESENE S/O DETANU, 22 YRS
32. HILMARAME S/O MOMO, 32 YRS
33. TEGICOR S/O TIMDO, 34 YRS
34. ABADA S/O SHOBISO, 30 YRS
35. YOHANES S/O ALAMU, 20 YRS
36. ABBAS S/O DESELING, 28 YRS
37. THADESAL S/O DIRAMOH, 26 YRS
38. STAGEI S/O THARDEL, 23 YRS
39. TSEGAYE S/O ADISE, 23 YRS
40. TESFAYE S/O WESHISO, 18 YRS
41. ABANEH S/O YOHANES, 20 YRS
42. ASFEW S/O DETABO, 19 YRS
43. TEMASGEN S/O YOHANES, 22 YRS
44. ASEFA S/O ERGUDO, 29 YRS
45. ASHURO S/O DE’LISO, 25 YRS
46. LAPSO S/O ABOSE, 30 YRS
47. DANIEL S/O ELISO, 25 YRS
48. SAREH S/O FITAMO, 26 YRS
49. SOLOMON S/O MANEBO, 18 YRS
50. ADIMASU S/O ABOSE, 20 YRS
51. ACHORE S/O TEMBEBO, 21 YRS
52. EYASU S/O ADEMASU, 18 YRS
53. FIKIRE S/O MALSEBO, 29 YRS
54. WOLDE S/O DEBISO, 25 YRS
55. SELAMU S/O DESTA, 23 YRS
56. SIYUNG S/O ASHURO, 25 YRS
57. TAREKU S/O ANIO, 23 YRS
58. DANIEL S/O FACHEL, 23 YRS
59. WAKU S/O DEBISO, 35 YRS
60. ADIMASU S/O FITIRE, 26 YRS
61. LIRI S/O IRISO.23YRS
62. BIRHAN S/O WLDE,20YRS
63. DAWITI S/O ANRE, 25 YRS
64. ARWEJE S/O TINDIDU,22YRS
65. SHOWICHO S/O ETIRO, 20 YRS
66. SELEMON S/O MATIUS, 20 YRS
67. TAMRAT S/O DASTA, 21 YRS
68. CAMRAT S/O AHENA, 32 YRS
69. DEMALKA S/O DOLEBO, 25 YRS
70. DENISE S/O WENDEMO, 24 YRS
71. DABABA S/O ABIO, 30 YRS
72. GERAMO S/O HERIMARIAM, 20 YRS
73. GEZAHA S/O EREGANO, 30 YRS
74. TISHELA S/O DEMISE, 21 YRS
75. WINDIMO S/O DEMISE, 28 YRS
76. ALAMU S/O LAPISO, 25 YRS
77. JOSEPH S/O WODIESU, 25 YRS
78. ABILNAT S/O TUMEBO, 22 YRS
79. TAKATAL S/O MARKOS, 22YRS,
80. YONAS S/O LILISO, 20YRS,
81. MUGRIETA S/O BUFAGHO, 26YRS.
82. WENDEMU S/O BEKERE, 22 YRS

MAREHEMU WALIOTAMBULIWA KUPITIA WENZAO WALIOKUWA HAI NI KAMA IFUATAVYO (X)

1.    ASAFA S/O ?
2.    MATOSI S/O KIMBAMBO
3.    TARAFA S/O ?
4.    MUREGETA S/O ?
5.    MADESE S/O BUKOLI
6.    ABRAM S/O ?
7.    LIRE S/O ABA
8.    SOLOM S/O ASIRIA
9.    YOHANES S/O BACHULE
10. JOSEPH S/O GAREMARIAM
11. ELIAS S/O NYACHULE
12. TEASAT S/O SEBETO
13. ASHINAFI S/O HAILE
14. ADEMASO S/O ABDILAH
15. TAMIRA S/O ?
16. BARATA S/O HERBETO
17. GILMA S/O DAMBARO
18. TERESAF S/O WEDESO
19. JOSEPH S/O MARIAM
20. TAFASA S/O KAMBAYA
21. ELIAS S/O ABETO
22. GETAUNI S/O ?
23. ASHARO S/O RETEGANI
24. TAFASI S/O ?
25. NAKANISI S/O ?
26. ALVIS S/O ?
27. LAISO S/O NASAMA
28. SHAWICHO S/O AGAFU
29. ALAMINO S/O BLAMU
30. ABARA S/O GERMANUS
31. DESTEL S/O DETAMO
32. WINDIMO S/O ?
33. HANDISO S/O BAILO
34. WUBISHETI S/O ?
35. BUZINE S/O ?
36. DESARE S/O ?
37. TADESA S/O WOLDEOMBA
38. FULGENCE S/O ?
39. FATAMA S/O ?
40. ABRAHAM S/O ?
41. NETA S/O ?
42. DANILA S/O
43. HAJAFAHAMIKA
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: