Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania kupitia kampuni ya Lino Ntenational Agency, Hashim Lundenga akizungumza na baadhi ya washiriki wa shindano la Redds Miss Kurasini jioni ya leo Mei 22,2012 wakati wa mazoezi yao yanayoendelea katika Ukumbi wa Equator Grill jijini Dar es Salaam. Redds Miss Kurasini imedhaminiwa na NAEEMS WAER , wauzaji wakubwa wa nguo za aina zote jijini Dar es Salaam wenye maduka yao Kariakoo na Mwenge, linataraji kufanyika Mei 25, mwaka huu ukumbini hapo. 
 Lundenga aliwataka warembo hao kujiheshimu maana urembo ni kazi kama zilivyo kazi nyingine na warembo wengi wanaojiheshimu na kuwa na tabia njema katika jamii huwa na mafanikio makubwa.
 Kamati hiyo pia ilihudhuria na Katibu Mkuu wake Bosco Majaliwa, Mkuu wa Itifaki, Albert Makoye, Ofisa Habari, Aidan Ricco na Ofisa wake Yason Mashaka.
Warembo wanaoshiriki shindano la Redds Miss Kurasini wakiwa katika Picha ya pamoja baada ya kuzungumza na Kamati ya Miss Tanzania. 

Wakati Nameems Wear wakiwa ni wadhamini wakuu, wakisaidiwa na Reds, Dodoma wine, Clouds FM, Lady Pepeta, Father Kidevu Blog, Jambo Leo, Aucland Tours & Safaris, Candy Bureau de Change, Flexip, PJ Amusement, Renzo Salon na Madishisha Video Production.

Aidha Jumla ya warembo 16 wamejitokeza kuwania taji la Redds Miss kurasini 2012, ambalo taji linashikiliwa na Top Model wa Miss Tanzania 2011, Mwajabu Juma.

Akiwataja warembo waliopo kambini na kunolewa na Mwajabu Juma akisaidiwa na Malkia wa vipaji wa Miss Tanzania 2011, Rose Hurbert ni Mariam Sadic (19), Johari Juma (20), Linda Deus (20), Irene Sostheness 20),Neemadoree Sylvery(29),Edna Magige (22), Lindanancy Joseph(20), Elizabeth Mkende (19), Betty Peter (22), Jennifer Njabili (18), Lilian Joseph (20), Farida Mrope (23),Christina Moses (20), Angle Gasper (19), Flaviana Maeda(22)      na Sia Kimambo (19).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

2 comments:

  1. UNATAKA WASICHANA WAJIHESHIMU,WAKATI WAMEKUKALIA MBELE YAKO NA KIGUO KIFUPI?

    ReplyDelete
  2. UNATAKA WASICHANA WAJIHESHIMU,WAKATI WAMEKUKALIA MBELE YAKO NA KIGUO KIFUPI?

    ReplyDelete