Na Pardon Mbwate na Felister Chubwa wa Jeshi la Polisi Kigoma
Mkazi mmoja wa Kijiji cha Katanga katika wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, Petro Masumbuko(37), amejeruhiwa viabaya kwa kupigwa risasi mbavuni na majambazi kisha kupora shilingi elfu saba na simu moja ya mkononi.
Kamanda wa Polisi mkoni Kigoma Kamishna Msaidizi ACP Frasser Kashai, amesema kuwa tukio hilo limetokea jana marija ya saa 2.00 usiku baada ya kundi la watu wenye silaha kumvamia Bw. Masumbuko nyumbani kwake na kumpiga risasi kabla ya kumpora fedha hizo pamoja na simu yake ya mkononi aina ya Nokia.
Kamanda Kashai amesema majeruhi amekimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Kibondo kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kiafya pamoja na matibabu huku Polisi nao wakiendelea na uchunguzi na kuwasaka watuhumiwa wa tukio hilo.
Wakati huo huo, Polisi mkoani Kigoma wameanza uchunguzi wa kifo cha mkazi mmoja wa kijiji cha Kazegunga kilichopo katika kata ya Msimba Bw. Riziki Issa Mahela(32), aliyekutwa huko kwenye eneo la Kahabwa mjini Kigoma akiwa ameuawa kwa kukatwa katwa kwa mapanga kichwani na mgongoni.
Kamanda Kashai, amesema kuwa Polisi watatafuta chanzo na sababu za mauaji hayo na kitu kilichomfanya marehemu asafiri kutoka katika eneo la kijijini kwake hadi katika mtaa huo ambako ameuawa.
Huyo ni mtu wa tato kuuawa katika mazingira ya kutia mashaka katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita ambapo watu wengione wane waliuawa katika matukio matatu tofauti huku wawili mtu na mkewe wakiuawa kwa tuhuma za imani za kshiirikina.
Kamanda Kashai amewaonya vikali wale wote wenye kuchukua sheria mkononi kwa kuwazuru hata kuwaua wengine kwa sababu zozote zile kuwa watapambana na mkono wa dola kwa vyovoyte iwavyo.
Amesema Makachero wake wamejipanga kuhakikisha kuwa kila mtu aliyehusika katika mauaji ya mmoja wa marehemu hao kuwa ni lazima akamatwe na sheria kuchukua mkondo wake.
Amewataka wananchi mkoani humo kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi hilo li kusaidia kufanikisha kukamatwa wa washukiwa wote wa mauaji hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: