Wa kwanza kushoto ni meneja Mauzo wa Airtel Zanzibar Hagai Samson na Meneja uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando wakifafanua jambo kwawaandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa viwango vipya nafuu vya mawasliano kwa wateja wa Airtel walioko zanziba (unguja na Pemba) ofa hiyo itajulikana kama Airtel Nusu shilingi na itawawezesha wateja wa Airtel kuongea kwa Gharama nafuu kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 4 usiku kwa NUSU shilingi tu kwa sekunde , na kuanzia saa 4 usiku hadi 11.59 asubuhi ni ROBO shilingi tu kwa sekunde Airtel-Airtel Pia wateja watafaidika na kupata huduma ya Internet bure usiku, wakwanza kushoto ni Meneja Mauzo wa Airtel kanda ya Pwani Bi Aminata Kieta.
Meneja uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akifafanua jambo kwawaandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa viwango vipya nafuu vya mawasliano kwa wateja wa Airtel walioko zanziba (unguja na Pemba) ofa hiyo itajulikana kama Airtel Nusu shilingi na itawawezesha wateja wa Airtel kuongea kwa Gharama nafuu kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 4 usiku kwa NUSU shilingi tu kwa sekunde , na kuanzia saa 4 usiku hadi 11.59 asubuhi ni ROBO shilingi tu kwa sekunde Airtel-Airtel Pia wateja watafaidika na kupata huduma ya Internet bure usiku, wapili kushoto ni Meneja Mauzo wa Airtel kanda ya Pwani Bi Aminata Kieta.
---

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imetangaza punguzo za gharama za kupiga simu kwa kiasi kikubwa ili kutoa fulsa na unafuu zaidi  kwa wateja wa Airtel wa malipo ya kabla walioko visiwani Zanzibar Unguja na Pemba kuendelea kufurahia huduma ya Airtel

Huduma hiyo mpya ijulikanayo kwa jina la Airtel Nusu Shilingi itawawezesha wateja wote wa Airtel walioko visiwani Zanzibar Unguja na Pemba kuwasiliana na wenzao waliopo ndani ya visiwa UNGUJA na PEMBA au kuwapigia waliotoka nje visiwa  kwa gharama nafuu sana ya NUSU shilingi kwa kila sekunde kwa wale wote wanaotumia mtandao wa Airtel-Airtel kuanzia 12asubuh hadi saa4 usiku.  Baada ya saa4 usiku hadi 5:59 mteja atafurahia ROBO shilingi tu kwa kila sekunde pamoja na intanet ya bure usiku mzima.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa Znz NUSU shilingi katika ofisi za Airtel Zanziba Mkurugenzi wa Airtel Tanzania Bw, Sam Elangalloor alisema "kutoa mawasiliano bora na nafuu nchini Tanzania ndio dhamira yetu kubwa.viwango nafuu tunavyozindua leo ni maalum kwa wateja wetu walioko zanziba na watakaoingia, lengo letu kufanya punguzo hili hadi NUSU shilingi kwa sekunde liko sambamba na ahadi  yetu Airtel nchini ya kutoa huduma za mawasiliano zenye ubunifu na ubora zaidi  ili kuwa suluhisho la kukuza uchumi na kutimiza uhitaji wa wateja wetu nchini kote.

Hivyo Zanzibar NUSU shilingi kwa sekunde Airtel kwenda Airtel ni kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 4 usiku, na kuanzia saa 4 usiku hadi 11.59 asubuhi ni ROBO shilingi tu kwa sekunde Airtel-Airtel pamoja na huduma ya Intanet bure usiku. Alieleza bw Elangalloor

Tunafahamu uhitaji wa mawasiliano ya intanet kwa sasa unauwiano sawa na huu wa kupiga au kuongea kwa simu na ndio maana tumeamua kufanya pia internet iwe BURE usiku mzima.

Airtel kwa sasa inaendeleza mkakati wake wa kusambaza mtandao wake wa 3G unaowezesha mawasiliano ya haraka katika Intanet (Data) kwa nchi zote za Afrika ambapo Mwaka huu wa 2012 Machi Airtel Tanzania ilifanikiwa kuzindua mtandao wa internet wenye kasi na ubora zaidi wa 3.75G. Airtel inaamini kuwa kujipanga kwake kwa kutoa mawasiliano bora ya kuperuzi mtandao yaani DATA hasa kupitia njia rahisi ya simu ya mkononi italeta maendelea makubwa sana kiuchumi, kijamii na utamaduni kwa wanaopata huduma hiyo bora ya Airtel 3.75G.

Kuanzia mwaka 2011, Airtel imeongeza minara mipya ya 3G zaidi ya 3,801 kwa Afrika nzima ambapo minara  303 tayari imejengwa ndani ya mwaka 2012 na kuanza kufanya kazi nchini Tanzania.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: