Maandamano ya wafuasi na wanachama wa CHADEMA wakimsindikiza "Aliyekuwa mbunge wao" wa Arusha mjini ndugu Godbless Jonathan Lema kuelekea viwanja vya Ngarenaro majira ya saa nane na dakika 15 ambapo hatimaye alihutubia wananchi. Mahakama imetengua ubunge wa Lema kutokana na kesi iliyofunguliwa na wanachama watatu wa CCM.

Godbless Jonathan Lema amekubali uamuzi wa mahakama na amesema haina haja ya kukata rufaa isipokuwa ATASHINDA TENA kiti hicho katika uchaguzi mdogo utakaoandaliwa na tume ya Taifa ya uchaguzi.
PICHA/HABARI NA SUBI
---
Habari na Woinde Shizza, Arusha

Mahakama kuu Mkoa wa Arusha imetengua matokeo ya Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini ambalo lilikuwa chini ya Bw Godbless Lema mara baada ya kukutwa na hatia ya kukiukia maadili wakati wa kampeni za uchaguzi za mwaka 2010.

Akitoa hukumu hiyo katika mahakama hiyo Jaji kutoka mahakama ya kanda ya Sumbawanga Jaji Mfawidhi Bw. Gabriel Rwakibarira alisema kuwa katika malalamiko 10 yaliyopelekwa na wafuasi wa chama cha mapinduzi (CCM) Mbunge Lema alikutwa na hatia. Jaji huyo alisema kuwa katika mikutano 60 ya kampeni ambayo alifanya Bw. Lema Mikutano 8 alikiuka maadili kinyume cha sheria na taratibu za uchaguzi jambo ambalo linafanya matokeo yake ya Ubunge yatenguliwe.

Alisema kuwa ndani ya malalamkiko hayo kumi ambayo yamewasilishwa mahakamani hapo alikutwa na hatia katika makosa 8 ambapo mawili hayakukubalika kwa mujibu wa sheria na taratibu za mahakama “kwa mujibu wa sheria na taratibu Lema amekutwa na hatia katika malalamikio na dondoo nane kwa hali hiyo akasema kuwa nabatilisha matokeo ya ubunge wa jimbo la Arusha Mjini na kwa hali hiyo taratibu nyingine zinatakiwa kuanza kufuatwa “aliongeza Jaji Gabriel.

Pia alifafanua kuwa kwa mujibu wa sheria namba 114 katika kifungu kidogo cha kwanza hadi cha saba cha sheria za uchaguzi msajili wa mahakama kwa kanda ya Arusha anatakiwa kukitumia kwa kuhakikisha kuwa anapeleka taarifa kwa tume ya uchaguzi juu ya kubatilishwa kwa matokeo hayo.

“Msajili wa mahakama anatakiwa kutumia kifungu hiki na kuhakikisha kuwa tume inakuwa huru kwa kuwa mpaka sasa tayari mahakama imeshatengua matokeo kwa mujibu wa sheria za mahakama” aliongeza Jaji Gabriel. Hata hivyo alisema kuwa bado Mbunge huyo ana nafasi ya kukata rufaa kwenye ngazi za juu za mahakama endapo kama hataridhika na mwenendo wa kesi pamoja na hukumu ambayo iliyotolewa ndani ya mahakama hiyo kwa muda wa siku 30.

Naye Bw. Lema alisema kuwa pamoja na kutenguliwa kwake kwa ubunge wa jimbo la Arusha mjini bado yeye ndiye, mbunge na hata kama uchaguzi utarudiwa ni wazi kuwa yeye ndiye atakayeshinda ingawaje hizo ni Mbinuza Viongozi wa juu Taifa la Tanzania (MAJINA TUNAYO) ambazo toka hapo awali alikuwa amezikataa.Bw. Lema aliongeza kuwa Mahakama kupitia kesi yake imeonesha wazi jinsi ambavyo wanavyobaka Demokrasia na suala hilo litawapeleka watu katika misitu bila kupenda na pia nchi itaingia katika machafuko.

Alifafanua kuwa mpaka sasa yeye ni jasiri wa hali ya juu sana na kwa hali hiyo atahakikisha kuwa anapambana kwa nguvu zote katika kutetea haki za wanyonge hata kama ametenguliwa ubunge wa Arusha Mjini. “Ninachoweza kusema ni kuwa nina moyo mkubwa sana kwani mimi nimepita katika mapito ya hali ya juu sana na pia aliyeniweka madarakani ni Mungu na wala sio hao viongozi wa ngazi za juu na ninapenda kuwatiamoyo kuwa hii hukumu ya kutengenezwa kama siyo ya kutengenezwa imekuwaje kila kiongozi anajua hii hukumu kuanzia juzi na jana” alisema Bw. Lema.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Bw. Freeman Mbowe alisema kuwa hiki ni kipindi kigumu sana kwao na pia ni kipindi cha mpito, pamoja na kuweka jazba pembeni badala yake chama hicho kinatakiwa kuonesha dunia, mahakama jinsi haki inavyopatikana Bw Mbowe alisema kuwa chama hicho hakiwezi kukataa ama kukuabali hukumu ya mahakama badala yake chama hicho kinalenga kutafuta haki siku ya Jumamosi katika viwanja vya NMC jijini hapa ambapo pia watashahuriana kabla na kasha kutoa tamko.

“Mimi naheshimu sana mahakama kwa kuwa inataratibu zake za msingi na kwa hali hiyo nawasihi sana wananchi kuwa watulivu kwa siku hizi mbili mpaka Jumamosi tutatoa hatma yetu kama tutakata rufaa au laa! na baada ya kushahuriana na viongozi na wanasheria wetu wa chama “aliongeza Bw Mbowe.

Kwa upande wa walalamikaji, ambaye aliongea kwa niaba ya wenzake Bw. Happy Kivuyo alisema kuwa mahakama imefanya uamuzi wa hali ya juu sana na imeonesha haki kwa kuwa Bw. lema alikuwa anatoa lugha za matusi na kuzalilisha sana.

Bw Happy alisema kuwa wao walichokuwa wanakitaka ni haki na wala sio Ubunge kwa kuwa hilo litakuwa ni fundisho hata kwa wagombea wengine ambao wanazalilisha watu kijinsia kwa madai kuwa wapo kwenye Kampeni.

“Napenda niwaambie wakazi wa mji wa Arusha kuwa malalamiko yetu hayakuwa ya kuchonga ila yalikuwa ni ya msingi wa hali ya juu sana na kwa hali hiyo mahakama imefanya uamuzi wa hali ya juu sana” alisema Bw. Happy.

Hata hivyo mara baada ya hukumu hiyo shuguli za mahakama zilifungwa huku kila kona ya jiji ikilindwa na Polisi wa kuzuia vurugu, huku shuguli mbalimbali za maendeleo zikisimama kwa muda kutokana na wingi wa watu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: