UTITIRI wa wafanyabiashara ndogondogo nchini unazidi kukua nchini, jambo linaloonyesha kuwa serikali imeshindwa kutatua tatizo la ajira nchini.

Pamoja na wafanyabiashara hawa maarufu kwa jina la wamachinga kuongezeka kwa kasi kubwa lakini wamekumbwa na kadhia za kunyang’anywa mali zao na mgambo au askari wa maeneo ya tawala zinazohusika kwa madai kuwa wanafanya biashara maeneo yaliyokatazwa au kutokuwa na vibali au kwa kutolipa ushuru.

Hawalipi kodi kwa kuwa mamlaka zinawapuuza na haziona hazina kubwa ya kundi hilo la kutunisha fuko la serikali na badala yake inaajiri mgambo kufukuzana nao bila kujua kuwa jeshi hilo linaoongezeka na mgambo hawatashinda kamwe vita hivyo. 

Dar es salaam pekee inasadikiwa kuwa na wamachinga 400,000. Huko mikoani nako idadi yao inazidi kukua kwa kuwa uchuuzi ndiyo ajira mbadala kwa wahitimu kutoka shule, vyuo na hata wanaaofukuzwa kazi au kustaafu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: