Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo ameagana na mabalozi wanne wapya
wanaoiwakilisha Tanzania nchi za nje wakati walipomtembelea ikulu jijini
Dar es Salaam leo asubuhi.Mabalozi hao waliapishwa hivi karibuni.
Mabalozi wapya walioagana na Rais Kikwete ni pamoja na Mhe.Philip Marmo
anayekwenda China, Mhe.Grace Mujuma anayekwenda Zambia, Mhe.Mohamed Haji
Hamza anayekwenda Misri na Mhe.Dkt.Batilda Burian anayekwenda Kenya.
Katika picha juu Rais Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete akizungumza na Balozi mpya wa Tanzania nchini China Mhe.Philip
Marmo ikulu jijini Dar es salaam leo aasubuhi.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Balozi mpya wa
Tanzania nchini Kenya Mhe.Dkt. Batilda Burian ikulu jijini Dar es Salaam
leo asubuhi.Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na balozi mpya wa Tanzania nchini
Zambia Mhe.Grace Mujuma Ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi (Picha
zote na Freddy Maro).
Toa Maoni Yako:
0 comments: