Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Sam Elangalloor akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa Airtel 3.75G hii leo jijini Dar es Salaa katika makao makuu ya Kampuni hiyo.
Beatrice Singano Mallya ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasilianowa Airtel akizungumza wakati wa uzinduzi huo hii leo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu Sam Elangalloor.
Mambo ya airtel internet 3.75G
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akielezea machache juu ya huduma yao mpya.
Meneja Maendeleo wa Bidhaa wa Airtel, Salum Madati akifafanua juu ya bidhaa hiyo mpya iliyozinduliwa hii leo.
---
Airtel Tanzania leo imepiga hatua kubwa katika kujenga na kukuza mtandao wa technoloijia ya 3.75G Africa kwa kuzindua rasmi mtambo wa 3.75G nchini Tanzania,ambapo Airtel itatoa huduma ya internet yenye ubora na kasi zaidi kwa watumiaji wenye simu zenye uwezo wa kutumia internet wawapo mahali popote.
Mkurungenzi Mkuu wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Sam Elangalloor alieleza” kukua kwa technolojia hii kutakuza ufanisi katika vyombo mbalimbali vya mawasiliano (multimedia), kwa kuwa 3.75G itatoa internet yenye ubora na kasi zaidi kwa kuwezesha wateja kufungua tovuti mbalimbali, kufanya maongezi ya simu kwa njia ya video , kuangalia TV, kutuma na kupokea barua pepe na pia kupata muziki kutoka kwenye tovuti kwa kutumia simu.
Teknologia ya 3.75G itatoa nafasi kwa wateja kupata mawasiliano ya data kwa njia tofauti na ya pekee kabisa, ndio maana leo Airtel tunajisikia fahari kuwa internet yetu ya 3.75G ni uvumbuzi na muendelezo wa mtandao (platform) wetu ili kuwawezesha wateja wa Airtel wote nchini kupata huduma ya internet au data yenye ubora wa hali ya juu pamoja na kasi zaidi”
Tunafanya ubunifu wa kuleta huduma zenye ubora zaidi katika mtandao kwa kuzingatia kuwa sasaivi dunia inauhitaji mkubwa sana wa huduma za kimtandao hasa kupitia simu ya mkononi
Ukirejea takwimu zilizofanywa na kampuni ya McKinsey & Co. Telecommunications zinaonyesha mpaka sasa kuna watumiaji wa simu za mkononi wapatao milioni 400 Afrika, na kwamba bara la Afrika ni moja kati ya soko linalokuwa kwa kasi zaidi huku soko la simu za mkononi likiendelea kukua na kupanuka zaidi na kufikia kutoa huduma za internet, huduma za benki kwa njia simu (mobile banking) na biashara kwa njia ya mtandao yaani (mobile commerce) .
Hivyo basi kwa kuzingatia hili, ndio maana Airtel tunaendelea na mikakati kama hii ya kuwaletea wateja internet yenye kasi zaidi ya 3.75G ambayo ni sambamba na lengo letu la kuendea kupanua mtandao ili kutoa mwanya wa mawasiliano kuwafikia wakazi wengi wa vijijini ambao walikuwa wamesahaulika na mapinduzi ya mawasiliano katika bara la Afrika.
“wote tunafahamu kuwa mawasiliano ni nyenzo muhimu kwa maendeleo ya jamii ya sasa lakini bado kunachangamoto kubwa sana katika kupata huduma hii kwa baadhi ya sehemu barani Africa.
Lakini tukumbuke Mawasiliano ni haki ya msingi kwa kila mtu na si vinginevyo hivyo kwa kupitia mtandao wa Airtel internet yenye kasi zaidi ya 3.75G ninaamini tutaweza kuunganisha idadi kubwa ya watu kwa kukuza mahusiano ndani na nje ya ya jamii zetu, kuendeleza na kuutangaza utamaduni wetu, pamoja na kupanua wigo wa wale wanaofanya biashara kupitia mtandao wa internet “ Aliongeza Elangalloor.
Ikiwa tayari mteja ameunganishwa na teknologia ya 3.75G simu yake itaonyesha 3.75G, HSDPA, WCDMA or HSPA. Hii inategemeana na Aina ya simu aliyonayo mtumiaji lakini kasi ya kuunganishwa ni yenye ubora zaidi.
Airtel itaendelea kuwekeza kwenye huduma ya data katika soko lake lote huku lengo likiwa ni kuwa mtandao mpana zaidi wa teknologia ya 3.75G katika bara zima, na itaendelea kutoa huduma bora na inayokidhi mahitaji ya watumiaji.
Toa Maoni Yako:
0 comments: