Katika jambo ambalo limeishangaza dunia hasa hapa nchini Tanzania ni suala la kualikana katika msiba (maziko), maana wengi huwa wanajua jambo la matatizo yanapotokea wanaoweza kuhudhuria ni watu wote halibagui dini wala kabila.
Familia ya Whitney Houston imewasikitisha maelfu ya mashabiki wa mwanamuziki huyo kutokana na kudai kuwa maziko yatafanyika kesho jumamosi kwa kuhusisha familia na wale watakaopewa mwaliko maalum tu na yataonyeshwa 'live' katika stesheni ya BET kesho tarehe 18.02.2012 saa moja na nusu usiku saa za Afrika Mashariki.
Sehemu waliyopanga yafanyike mazishi hayo ina uwezo wa kuchukuwa watu 1,500 wakati awali kulikuwa na taarifa kuwa zoezi la kuuaga mwili lilikuwa lifanyike katika Ukumbi wa Prudential Center unaochukuwa watu 18,000.
Mume wa zamani wa marehemu, Bobby Brown ana uwezekano wa kukosa kuhudhuria maziko kwa kile kinachodaiwa kuwa familia haimuhitaji na mpaka sasa haijampatia mwaliko.
Bado kuna wingu kubwa la maswali likiwa limetanda juu ya kifo chake kwani watu wa karibu na marehemu wameeleza kuwa siku chache kabla ya umauti kumfika alisema anataka kuonana na Yesu na alikuwa akisissitiza juu ya hilo pia shoo yake ya Mwisho kuifanya alivaa nguo nyeusi tupu.
Peter Tatchell ambaye ni mtetezi wa haki za watu wa jinsia moja wenye uhusiano wa kimapenzi aliandika katika mtandao wake kuwa, Whitney aliwahi kuwa mmoja wao lakini alifanya hivyo kwa siri miaka ya nyuma.
Toa Maoni Yako:
0 comments: