Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akizungumza leo na Madaktari kufuatia sakata la mgomo wao uliodumu kwa kipindi cha zaidi ya wiki mbili sasa wakati alipofika kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam kwa lengo la kukutana nao na kusikiliza malalamiko yao.Pia kutokana Malalamiko ya Madaktari hao ya kutokuwa na imani na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Blandina Nyoni pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali,Dkt. Deo Mtasiwa.Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda amesema amewafuta kazi wakuu hao kuanzia leo hii kutokana na kuonekana kuwa wao ndio kiini cha mgogoro huo ambao umekuwa ukisababisha matatizo makubwa kwa taifa.Waziri Mkuu amewataka Madaktari waunde kamati maalumu ambayo itakusanya mapendekezo ya madaktari wote na kumpelekea yeye ili aweze kuyafanyia kazi,huku akiwataka Madaktari hao kurudi kazini na kuendelea na majukumu yao kama ilivyokuwa hapo awali.

Madaktari wakimuaga waziri mkuu mara baada ya Waziri Mkuu Piter Picha kuongea nao.
 Sehemu ya Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakimsikiliza Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda wakati akizungumza nao leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Hospitali hiyo leo.

Baadhi ya Madaktari wa Muhimbili wakizungumza huku umati wa madaktari wengine ukiwa umetulia kusikiliza. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: