Manusha Sarawan akielezea mchakato wa kumpata Rose Muhando ulivyofanyika.
Mwanamuziki wa nyimbo za Injili, Bahati Bukuku (kushoto,) na wanamuziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul ‘Diamond’ na Ally Kiba (kulia) wakisikiliza kwa umakini kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Kampuni ya bidhaa za Sony Barani Afrika kupitia vifaa vyake vya muziki imemteua mwanamuziki wa nyimbo za Injili hapa nchini, Rose Muhando, kuwa mmoja wa mabalozi wake. Uteuzi huo umetangazwa leo na Mkurugenzi wa Mambo ya Masoko, Manusha Sarawan, katika mkutano na wanahabari uliofanyika Hoteli ya Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
Manusha alisema mchakato wa kumpata balozi huyo ulishirikisha wanamuziki wakongwe zaidi ya 130 barani hapa.
PICHA : RICHARD BUKOS,/GPL
Toa Maoni Yako:
0 comments: