Tulitegemea kwa wasanii wakubwa kama  Ambwene Yesaya a.k.a A.Y  kama anavyofahamika  kwa mashabiki wengi wa muziki, angekuwa ni mfano wa kuigwa na wanamuziki chipukizi hapa nchini, ila badala yake ameonekana kutokuwa na discipline na kikwazo kikubwa cha kukua kwa muziki wa reggae na ragga hapa nchini.

Sisi kama Jahson na Susu hatuwezi kujifunza lolote kutoka kwa msanii huyo (A.Y) kwa sababu amekuwa ni mtu alionyesha utovu wa nidhamu ya hali ya juu mara kadha wa kadha  mfano.

Wengi tunamjua A.Y kama msanii wa hip hop lakini mwaka 2010 aliwahi kushindania tunzo ya mwanamuziki bora wa reggae na hatimaye kupata tunzo hiyo na kuichukua kwa mbwebwe zote na pia mwaka huu 2012 amewekwa kwenye category  ya ragga na nina imani atapata tu tunzo hiyo kutokana ma madhaifu yaliyopo katika uandaaji wa tunzo hizo za Kilimanjaro Music Award.

Bushoke alikuwa mfano mzuri sana wa kuigwa alipopewa tunzo ambayo hakustahili na kuikataaje, A.Y kwa nini alikubali tunzo hiyo? Na ki ukweli haikumstahili

Ki ukweli wasanii kama A.Y wanatuvunja moyo sana sisi wasanii ambao tunaofanya muziki huo pamoja na mashabiki wa muziki huo wa reggae na ragga na kwa taarifa yake tu AY asijidanganye kwa wingi ama uchache wa kura hizo anazopata katika kinyang’anyilo hicho, asidhani kama anapigiwa na mashabiki wa Reggae na ragga, no huo ni uongo mtupu ni mashabiki wake wa hip hop ndiyo wanaomuwezesha so anawakanganya wapenzi wake kiukweli.

Sisi kama washikadau wakubwa wa muziki huu wa Ragga na Reggae tumesikitishwa sana kwa mapungufu makubwa ya msanii huyo AY kuzidi kukumbatia ujinga unaofanyika kila mwaka sijui anataka tujifunze nini msanii huyo bwana Ambene yesaya.

Atumchukii AY hapana ila tunajalibu kuweka mambo wazi na kutoruhusu ujinga huu kuendelea maana kuna wakati ataimba Taarabu na Bolingo na watamuweka kwenye category hiyo na atachukuwa, inawezekana kabisa akawa anauwa muziki wake ama anawagawanya mashabiki wake kwa kutotulia kwenye style ya muziki wake, na kuwa kama Inzi anavyotua mara kwenye embe bovu mara kwenye kidonda mara jalalani, atumuelewi bwana A.Y

Tungependa washikadau wa wakubwa wa muziki huu walione kama hili ni tatizo na walikemee kwa nguvu zote ili Tanzania iwe na ukomavu wa muziki huu tofauti na hapo tutakuwa tunapiga kwata bila kusonga mbele.

Sisi tumeshafanya nyimbo kama Heat na Show me some love ambazo zimefanya wema katika vituo mbalimbali lakini tumeenguliwa kwenye tunzo hizo hii inakatisha tamaa sana, lakini sisi hatutokata tamaa na wala haitufundishi uonga wa kupigana na kitu ambacho tunaamini tunakifanya vema kabisa japo kuna wasanii wengi wakali waliamua kuachana na muziki kwa ajili ya mambo ya kinyama kama haya.

Shabiki wetu jaribu kuingia kwenye youtube na usearch Jahson & Susu ama Jahson Tanzania alafu utoe coment je tunastahili kunyimwa tunzo hizo?
(Nyimbo yenyewe ndiyo hii)

Asanteni ni sisi Jahson na Susu

(Hayo ni maoni ya wasanii hao waliyotuma kwangu na mimi ujumbe nimekufikishia mdau).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: