Na Mwandishi  Wetu

Watanzania zaidi ya milioni 1, wamefaidika kwa namna moja au nyingine, na mradi wa Elimu ya Afya ya Uzazi na  kuwajengea uwezo wa kujitegemea vijana,  wa kike, walioko katika sekta isiyo rasmi ulioendeshwa na Shirika la DSW  la Ujerumani kwa kushirikiana na 4H  na Umati.

Hayo aliyabainishwa na  Mkurugenzi Mkazi wa DSW  nchini Tanzania Bw. Peter Owaga, wakati wa semina ya siku moja ya kuhitimisha mradi huo, uliodumu kwa miaka 4, iliyofanyika mjini Moshi hivi karibuni.

Bw. Owaga alisema  mradi huo, uliofadhiliwa na fedha kutoka Jumuiya ya Ulaya (EU) umewajengea uwezo wa kiuchumi vijana wa kike zaidi ya 5,000 katika wilaya tisa  walio katika sekta isiyo rasmi toka mikao ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga kwa kuwapatia elimu ya afya ya uzazi, kundi rika,  elimu ya ujasiliamali na kuwapatia mitaji na vifaa mbalimbali mfano seti ya komputa kwa ajili ya miradi midogo midogo ya kiuchumi hivyo kuwawezesha kujitegemea na kusaidia familia zao na kujenga uchumi wa taifa.

Bw. Owaga aliishukuru Jumuiya ya Ulaya na wadau wengine kwa kuufadhili mradi huo, na kutoa wito kwa wadau mbalimbali zikiwezo asasi za kiraia, kusaidia juhudi za serikali katika kuwawezesha vijana kujiajiri na kujitegema kwani wao ni moja ya sehemu muhimu ya jamii inayokabiliwa na changamoto mbalimbali ukiwemo  hatari ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa na Ukimwi.

DSW  ni shirika la Ujerumani linalojihusisha na utoaji wa elimu ya afya ya uzazi, na lilianza shughuli zake nchini Tanzania mwaka 1996.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: