Band inayovuma kwa sasa nchini Tanzania, kwa uchezaji wao wa staha na sauti zenye kusikika vyema.

Kiongozi wa Glorious Celebration Band, Emmanuel Mabisa, akiongea kuelezea machache kuhusu kazi yao na malengo waliyonayo katika kuujenga mwili wa Kristo.

“Maono yetu ni kufanya huduma mashuleni na vyuoni kwa ajili ya kuwahubiria Vijana Habari njema za Kristo, na pia kufanya matamasha makubwa mbali mbali” alisema.

Aidha kundi hilo linaundwa na waimbaji mahiri wanaowahi kusikika awali wakiwa mmoja mmoja kwenye soko la muziki wa injili na wengine chipukizi wanasikika sasa kwa mara ya kwanza. Band hiyo inalelewa na msimamizi mkuu Bishop Mwakang’ata wa Full victory Gospel Church ya Chang’ombe Temeke, Dar es salaam.

Waimbaji wengine wanaounda kundi hilo ni Angel Bernard ambaye ndiye mweka hazima, Chaka Mtunguja Katibu wao, Jesca Honore, Nice Marandu, Davina, Risper, Ima Malisa, Emmanuel Materu, Emmanuel Gripa, Daniel Kibambe, Arone Botto, David Silomba, Ester Peter, Paul Mwakanyamale na Mercy Denis.

Pia kuna mtumishi wa Mungu Rulea Sanga ambaye yeye sio mwimbaji ila ni mhamasishaji wa band hiyo kwa njia ya mtandao, Mungu bado hajampa karama ya uimbaji, ila anasema ana ndoto za kuwa mwimbaji wa kimataifa kwa utukufu wa Mungu.

Kwa sasa wanajiandaa kurekodi Live DVD mapema mwezi wa sita mwaka 2012! Hapo awali wamerekodi video ya album yao ya kwanza NIGUSE.

Mpaka sasa wametimiza mwaka mmoja tangu wameanzisha bendi yao na wametoka na album ya NIGUSE…. hata hivyo kama watu walivyozoea kila Ijumaa kuwaona THE ATRIUMS HOTEL, kwa sasa itakuwa wanamtukuza Mungu kila ijumaa ya mwisho wa mwezi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: