Jina kamili; JUSTINE ERICK KOBERO,

Jina la kisanii; AMAZONE.

Nimezaliwa; DSM,

Natokea; MOROGORO.

Naishi: KIJITONYAMA, Jijini Dar es Salaam

Nimeanza muziki mwaka 2006, mwaka 2009 nikafanikiwa kujiunga na THT, na nikapata mafunzo chini ya walimu, wangu 2, mmoja anajulikana kwa jina la teacher HAKI{mwalimu msaidizi}, na teacher KARDINAL GENTO, huyu ndiyo mwalimu wangu mkuu.

Nyimbo yangu ya kwanza kuitoa redioni inaitwa CHECHERUMBA, ambayo imeshaanza kusikika katika stesheni mbali mbali za redio hapa nchini Tanzania, nilirekodi wimbo huo katika studio iitwayo KIRI RECORDS, chini ya producer C9.

Uzoefu wangu katika muziki nimefanikiwa kuimba katika bendi ya THT kwa takribani miaka 2, nimezunguka mikoa ya Mwanza, Tanga, Morogoro na ikiwemo DAR-ES-SALAAM pia hii yote katika kufanya show za kijiimarisha kimuziki.

Kutokana na hayo sasa AMAZONE nimeamua kutoa nyimbo yangu mwenyewe inayojulikana kwa jina la CHECHERUMBA, Kwa hakika ni kazi ambayo ipo tofauti sana tena sana, endapo utapata fursa ya kuisikiliza kazi hiyo ndio utajua nini namaanisha, asante sana, MUNGU ibariki CHECHERUMBA, MUNGU mbariki kijana wako  AMAZONE.
Sikiliza nyimbo yake hapa chini::
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: