Na Ben Komba-Pwani.
WIZARA inayohusika na masuala ya afya inahitajika kuwa macho na mipira ya kiume inayosambazwa na PSI, maarufu kwa jina la SALAMA, Ambapo siku za hivi karibuni imekuwa inashuka ubora wake siku hadi siku kutokana na kutokukaguliwa ipasavyo na wakaguzi husika katika suala zima la kuhakikisha maambukizi dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI yanapungua au kufutika kabisa.
Katika utafiti niliofanya nimegundua katika kila kondom za salama 3 ambazo zinauzwa kwa watu wanaohitaji kufanya ngono basi mbili zitapasuka hata kabla ya pambano lenyewe kushika moto, katika hali kama hiyo kuna uwezekano mkubwa wa maambukizi ya ugonjwa huo kuongezeka kutoka na kitendo chenyewe kupendwa na wanadamu walio wengi hususan maskini ambo ndio wanalengwa zaidi na kondom hizo ambazo nyingi zake ugawiwa bure.
Kinachonisukuma kuandika makala hii ya kiukweli ni maswali kadhaa ambayo nimejaribu kuyauliza kwa wafanyakazi wa baa, nyumba za kulala na wafanyabiashara za ngono wa maeneo mbalimbali ambao kwa njia moja au nyingine nimesaidiwa kujua ubora wa mipira ya kiume ambayo imesambazwa katika maeneo mbalimbali na kuigharimu serikali na wafadhili mamilioni ya shilingi.
Ambapo mmoja wa mfanyabiashara wa ngono niliyeongea naye kwa masharti asitajwe jina lake amesema wao kwa upande wao wamekuwa makini kusikiliza hatua kwa mdundo unaosababishwa na mapenzi na hivyo inakuwa rahisi kwao kugundua mara mpira huo unapopasuka, nilipotaka kujua hasa kwa nini mipira hiyo inapasuka wakati wa mechi, alinijibu kwa kifupi kuwa mara nyingi wao wanatumia mipira ya shilingi 1500/= aina ya ROUGHRIDER.
Sasa kwa msingi huo kwa hali ya sasa ya kiuchumi kuna hatari ya wananchi wengi wenye kipato cha chini kuwa lengo kubwa la ugonjwa wa UKIMWI, na hasa kutokana na mchezo wa ngono kuwa kitu muhimu kijamii na kuongoza kwa kuwa na wapenzi na wachezaji wengi kama utafiti unavyojionyesha ambapo washiriki wake haujalishi iwapo muhusika ni mlemavu au hana akili nzuri, katika hali hiyo inakuwa ni vigumu kwa tatizo hilo kupungua hata iweje kiana kwamba kuna mbinu za makusudi za kusambaza ugonjwa huo, toka siku hizi mashirika yanayojifanya kujishughulisha na UKIMWI wanatumia ugonjwa huo kujinufaisha binafsi.
Kutokana na kuonekana kuna mapungufu kuhusiana na maambukizi ya ugonjwa huo katika ripoti iliyotolewa mwsaka jana, hiyo kwa upande wa mashirika yasiyo ya kiserikali yanayojishughulisha na UKIMWI, kwani hiyo kwao ni habari mbari mbaya ambayo mwisho wake fedha zinazotolewa na wafadhili zitapungua na hivyo kuwafanya wachache wanaonufaika na fedha hizo maisha kuwaendea kombo.
Suala hilo linafanana kidogo na lile suala la ugonjwa wa Tauni uliokuwa unawasumbua sana wakazi wa wilaya ya Lushoto mpaka pale ilipobainika kuwa kuna mbinu chafu juu ya mlipuko wa ugonjwa huo mara kwa mara na serikali ikawa inapeleka fedha nyingi ili kukabiliana ugonjwa huo hatari ambao uliua mamilioni ya watu katika karne ya 17 na 18, ambapo mara ya kubainika mbinu hizo ugonjwa huo kwa sasa umekuwa historia.
Tukizingatia mfano huo ambao kuna baadhi ya wajanja mtoto nao wanataka ku adopt katika karne hii ya sayansi na teknolojia tukiwa siku za mwisho mwisho kabisa hapa ulimwenguni ambapo inasemekana hata ukifanya vipi hakuna mwenye agenda ya kubaki toka wote tupo katika TRANSIT to NOWHERE na wengine wakiaamini wapo hapo ili kwenda mbinguni au Jehenamu.
Kwa kuzingatia hilo nikiwa mmoja wa wadau wakubwa wa mapambano dhidi ya ugonjwa hatari wa UKIMWI, nasikitishwa na hali hiyo hasa kwa kile kinachoonekana kama kuna baadhi ya ya wajanja watoto nikiwa na maana wengi walio kule ni watoto wa viongozi wetu wamegeuza suala hilo kama dili la kujibnufaisha kwa kununua kondom zenye ubora dhaifu na kuzisambaza kwa wananchi huku, huku wakijifanya weamenunua kondom hizo kwa bei kali, na kwa sababu inakuwa dili basi moja kwa moja walipaji utekelza malipo mara moja na mchezo umekwisha, ili hali watanzania hususan wa kipato cha chini wakiendelea kufariki dunia kwa ugonjwa huo.
Kunahitajika mabadiliko makubwa upande wa taasisi hasa FHI, PSI na wengine zinazopambana na maambukizi ya ugonjwa huo kutumia uwezo wake kama serikali ili kupambana na ugonjwa kwa kuanzia na safu ya wafanyakazi wa mashirika hayo na kupitia upya mikataba yao ya kazi katika kuhakikisha hakuna uchakachuaji wa makusudi unaofanywa na waroho wachache ambao tunawajua mpaka majina yao na mbinu zao wanazotumia.
Na ingekuwa vyema iwapo fedha lukuki zinazotumika kupelekwa katika mashirika yanayoendesha miradi hewa inayohusiana na UKIMWI, kusitishwa na kupeleka fedha katika kununua kondom zilizo bora katika kupambana kiukweli na athari zinazoweza kusababishwa na ugonjwa huo, badala ya kupeleka fedha nyingi kwa ajili ya matangazo ya mipira feki ya KONDOM ambayo baada ya miaka 10 itasasababisha balaa kubwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments: