Spika wa Bunge, Mhe. Anne Makinda, amewausia wakulima kote nchini, na haswa vijana, kutoendekeza sana siasa baada ya mwaka wa uchaguzi, na badala yake wajikite zaidi katika kilimo na shughuli mbalimbali za uzalishaji mali, na kuonya kuendekeza siasa wakati wote, kutawaletea umasikini.
Mhe. Makinda, ambaye pia Mwenyekiti wa Bodi ya Chai Tanzania, ameyasema wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Hati Miliki za Kimila, kwa wakulima wa zao la chai zilizofanyika mwishoni mwa wiki, hayo mwishoni mwa wiki mjini Njombe, mkoani Iringa.
Mhe. Makinda amesema, kipindi rasmi cha kupiga siasa, ni wakati wa mwaka wa uchaguzi, uchaguzi ukishamalizika, kupiga siasa inakuwa basi, na watu wanatakiwa kurejea katika shughuli zao za kilimo na uzalishaji mali, wale wanaoendekeza kupiga siasa wakati wote, wanajiletea umasikini.
Hapa nina mnukuu, “ Mimi nawaambie siasa tutafanya wakati wa uchaguzi, achene kufanya siasa kwa miaka yote mitano tutakufa masikini, huo ni mchezo wa umasikini, achene mchezo wa umasikini”, mwisho wa kunukuu.
Nae Mratibu wa Mkurabita, Bw. Ladislaus Salema, aamesema mradi huo wa kuwawezesha wakulima wadogo wa chai, unaoendeshwa kwa ushikiano kati ya MKURABITA, Bodi ya Chai Tanzania, na Chama cha Wakulima wadogo wa Chai Tanzania ambapo MKURABITA kwa upande wake, imejipanga kurasimisha mashamba ya wakulima kote nchini wanaoshughulika na kilimo cha mazao ya biashara.
Naye Mkurugenzi wa Urasimishaji wa MKURABITA, Bw. Steven Rusibamayila, Amesema wakulima zaidi ya 300, toka vijiji 46, walikabidhiwa hati zao za kimila za kumiliki Ardhi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: