Siku moja mara baada ya majambazi kuvamia gari ya abiria aina Land Cruser yenye namba za usajili T 853 BLF na kujeruhi watu sita na mtu kufariki, Jeshi la polisi mkoani Rukwa limeanza kuwasaka watu hao katika milima ya Muze na vijiji jirani yanakodhaniwa kukimbilia majambazi hayo huku wananchi wakitakiwa kutoa taarifa pindi watakapopatikana.
Oparesheni hiyo inayoongozwa na kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa Isuto Matage imeanzia eneo ambalo waliteka gari hilo na kuendelea katika vijiji vya bonde la ziwa Rukwa nyumba kwa nyumba ili kuwabaini majambazi hao.
Katika vijiji vya Mwale na mto wisa Kamanda Isuto anakutana na vikundi vya vijan na wanachi ili kutoa elimu ya ulinzi shirikishi ikiwa ni moja ya mbinu ya kuwapata majambazi hao wanaosadikiwa kutoka nchi jirani.

Toa Maoni Yako:
0 comments: