Baada ya kuripotiwa kuwepo kwa mgomo kwa madaktari katika baadhi ya hospitali jijini DSM hapa mjini DODOMA katika hospitali ya Rufaa ya mkoa Madaktari na wafanyakazi wengine wa hospitali hiyo wanaunga mkono
mgomo huo na kusema hawatafanya kazi kama ilivyo kawaida isipokuwa watatoa huduma za dharula tu.
Tamko la kuwepo kwa Mgomo huo unaodaiwa kutokuwa na ukomo limetolewa na viongozi wanaoshughulikia madai ya watumishi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa DODOMA katika mkutano uliojumuisha madaktari na wafanyakazi wote wa Hospitali hiyo ya rufaa .


Toa Maoni Yako:
0 comments: