Naibu waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Aggrey Mwanri ameagiza mkandarasi Josephat Rweyemamu wa kampuni ya Prutal ya mjini muleba asipewe kazi yoyote ya ujenzi katika halmashauri ya wilaya ya muleba mkoani kagera kufuatia mkandarasi huyo kujenga nyumba kumi za watumishi wa halmashauri hiyo chini ya kiwango.

Waziri Mwanri ametoa agizo hilo kwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Muleba Oliver Vavunge baada ya kukagua ujenzi wa nyumba hizo ambao umegharimu shilingi million mia tatu na kubaini kuwepo kwa kasoro kadhaa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: