MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

LEO USIKU:
Maeneo ya Pwani ya kusini, Morogoro(kusini) yanatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache. Maeneo ya mikoa ya Lindi, Morogoro( kaskazini), Pwani ya kaskazini yanatarajiwa kuwa na hali ya mawingu, mvua na ngurumo katika baadhi ya maeneo. Maeneo ya ukanda wa ziwa Victoria hususani mkoa wa Mara yanatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi na ngurumo katika maeneo machache Maeneo mengine ya nchi yaliosalia yanatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi na makavu kwa ujumla.

KESHO MCHANA:
Maeneo ya ukanda wa ziwa Victoria hususani mikoa ya Mara na Shinyanga, nyanda za juu  kusini magharibi,maeneo ya mikoa ya Ruvuma, Kigoma, Tabora, Morogoro(kusini) yanatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua. Maeneo ya Pwani yote, maeneo ya mikoa ya Morogoro(kaskazini), Pwani, nyanda za juu kaskazini mashariki, kati mwa nchi pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba yanatarajiwa kuwa na hali ya mawingu, mvua na ngurumo katika maeneo mengi na vipindi vifupi vya jua. Maeneo ya  mikoa ya Kagera naMwanza yanatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, ngurumo katika maeneo machache na vipindi  vya jua.

UNYEVUNYEVU KWENYE HEWA:
Kiwango cha juu cha unyevunyevu kwa Dar es Salaam kinatarajiwa kuwa asilimia 100 na kiwango cha chini kinatarajiwa kuwa asilimia 64. Kiwango cha juu cha joto kwa Dar es Salaam kinatarajiwa kuwa nyuzi joto 30°C na kiwango cha chini kinatarajiwa kuwa nyuzi joto 25°C.
Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 20 kwa saa kutoka kaskazini mashariki katika pwani yote.
 
Hali ya bahari: Inatarajiwa kuwa na mawimbi madogo madogo.

Matazamio kwa siku ya Alhamisi: 29/12/2011. Mabadiliko kidogo.

Utabiri huu umetolewa leo tarehe 27/12/2011.
Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: