Hii ndiyo picha ya ajali aliyoipata Ally a.k.a Daxx eneo la Victoria jijini Dar es Salaam tarehe 25/5/2011 siku ya Krismasi ambapo alikuwa kwenye Taxi akitokea nyumbani kwake Kinondoni jijini Dar es Salaam. Ambapo katika ajali hiyo dereva wa hiyo taxi Hassan alifariki baada ya kukimbizwa hospitali. Akisimulia mkasa wenyewe jinsi ajali hiyo ilivyotokea Ally alisema kuwa wakati wanaelekea Sinza kupitia Victoria walishtukia gari aina ya Prado imetokea upande wa barabara ya tatu huku ukiwa speed kali na kuwagonga upande wa dereva na yeye kutoa salama bila kupata hata jeraha lolote. Dereva amezikwa jana tarehe 26.12.2011 nyumbani kwao Bunju jijini Dar.
Home
Unlabelled
PICHA YA AJALI ALIYOPATA ALLY A.K.A DAXX SIKU YA X-MASS
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments: