Barabara ya kuelekea standi kuu ya mabasi ya mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro.
  Standi kuu ya mabasi ya mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro.
 ...Mnara wa saa ambao ndiyo kielelezo kikubwa cha mji wa Moshi.
...Mnara wa askari ambao pia unaonyesha ishara ya 'Maji ni Uhai'
...Soko kuu la Mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro.
Mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo kwa mbali unaonekana Mlima Kilimanjaro.
Mji wa Moshi wakati wa asubuhi.
Angalia jinsi miji ya mkoa wa Moshi mkoani Kilimanjari ilivyo misafi.
...ukungu ukiwa umetanda
...mji umepangika
...mitaa nayo imekaa vizuri
 Mlima Kilimanjaro unavyoonekana wakati wa asubuhi kutokea mji wa Moshi.

Mkoa wa Kilimanjaro ni kati ya mikoa 21 ya Tanzania Bara, ambao ulioanzishwa rasmi kwa Tangazo la Serikali Na. 450 la mwaka 1963 ukiwa na Wilaya za Kilimanjaro na Pare. Kabla ya hapo eneo hilo linaloitwa Mkoa wa Kilimanjaro lilikuwa sehemu ya Jimbo la Kaskazini (Northern Province) lililokuwa linaundwa pia na wilaya za Arusha na Mbulu; wakati wilaya ya Pare ilikuwa sehemu ya Jimbo la Tanga (Tanga Province).

Mkoa huu unayoidadi ya watu wanaofikia 1,381, 149 ambao wanalijaza eneo la Kilometa za mraba zipatazo 13,309 ambazo ni sawa na maili za mraba zipatazo 5,139.

Wakati nchi ya Tanzania inapata Uhuru tarehe 09.12.1961 Mkuu wa Jimbo la Kaskazini (Provisional Commissioner) alikuwa Mheshimiwa PC Edward Barongo ambaye alitawala hadi 1963, na alipokelewa na Mheshimiwa Peter Kisumo, Mkuu wa Mkoa wa kwanza wa Mkoa wa Kilimanjaro. Kwa mantiki hiyo Mkoa umetimiza miaka 38 tangu kuanzishwa kwake ukiwa umeongozwa na Wakuu wa Mkoa 18 hadi hivi sasa.

Mkoa wa Kilimanjaro una eneo dogo la utawala lenye kilomita za mraba 13,209, lakini ukiwa na msongamano mkubwa wa watu, vivutio vingi vya utalii mojawapo ukiwa mlima Kilimanjaro, wasomi wengi, miundombinu mizuri na ya uhakika, wachapa kazi ambao wanajituma katika kazi za kitaalamu na ujasiriamali, vyote hivi vikiwa ni vichocheo vikubwa vya maendeleo yake.

Mkoa wa Kilimanjaro una makao yake makuu katika mji wa Moshi, unayo majimbo ya uchaguzi yanayofikia (6) ambayo ni pamoja na majimbo ya Moshi Mjini, Moshi Vijijini, Vunjo, Siha, Hai na Mwanga.

Iii Napenda kuwapongeza viongozi wakuu wa mkoa huu 18 waliotangulia hadi kufikia mwaka huu 2011; kwani ndio walioweka misingi bora na imara ya maendeleo yaliyofikiwa hivi sasa, kama inavyoonyeshwa kwenye mafanikio kwa kila sekta katika taarifa ya mkoa.

Shukrani za dhati kwa serikali katika jitihada zake za kufikisha huduma na maendeleo kwa wananchi wa mkoa huu kupitia ngazi mbali mbali za kiutawala kuanzia ngazi ya Mtaa/Kitongoji, Kijiji, Kata na Halmashauri/Wilaya.

Mkoa wa Kilimanjaro una fursa nyingi za kimaendeleo ambazo zinawezesha uwekezaji unaotokana mazingira mazuri yaliyopo sasa hivi kama vile:-

(i) Miundombinu ya kuaminika na mawasiliano kama vile mtandao mzuri wa barabara za lami na changarawe zinazopitika kwa vipindi vyote vya mwaka;

(ii) Njia za mawasiliano ya Simu, Viwanja vya Ndege kikiwepo kiwanja cha Kimataifa KIA na viwanja vidogo vya Moshi Mjini na kile cha Utalii Same na njia ya Reli ya Moshi - Arusha – Dar es Salaam;

(iii) Upatikanaji wa kuridhisha wa huduma za tiba, maji, umeme na elimu;

(iv) Upatikanaji wa huduma na vivutio vya utalii kama vile Mlima Kilimanjaro, Hifadhi za Wanyamapori za Kilimanjaro na Mkomazi, misitu ya asili, mazingira yanayovutia tamaduni za asili na mapango ya kale;

(v) Uwepo wa vyombo vya kifedha kukidhi haja kama vile benki 13, SACCOS 217, mifuko ya hifadhi ya jamii na asasi nyingine ndogo ndogo za fedha kama vile vikoba;

(vi) Ulinzi na usalama wa kuridhisha.

Nina uhakika tukiweza kuimarisha mazingira haya mazuri ya uwekezaji na kuboresha miundombinu iliyopo sasa, Mkoa unayo nafasi nzuri ya kupiga hatua kubwa zaidi ya kimaendeleo katika miaka 50 ijayo. Hii ikiwa ni pamoja na kutumia ardhi ndogo tuliyo nayo kikamilifu kwa kujenga majengo kwa kwenda juu (vertical expansion) badala ya ujenzi wa kusambaa (horizontal development);

(iv) Mafanikio haya yamepatikana kutokana na ushirikiano na mshikamano kati ya viongozi mbali mbali wakiwemo viongozi wa serikali, chama, dini na wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro.

“TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE”
                                    
N:B Unaweza kusoma ripoti kamili ya mkoa wa KILIMANJARO,  BONYEZA HAPA
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: