Tigo, mtandao wa simu za mkononi unaoongoza Tanzania, leo umetangaza kuwa unapanua mtandao wake wa 2G na wa 3G kwa kuboresha vituo vyake vilivyopo na  kuongeza vituo vipya vya urushaji wa huduma za mtandao Tanzania nzima. Uboreshaji huo utaongeza uwezo, uharaka wa muitikio na ubora wa mtandao, na utatoa huduma zilizoboreshwa kwa wateja wake. 

“Kitu cha msingi katika mkakati wetu wa ukuaji kimekuwa ni kutilia mkazo suala la utoaji wa huduma zinazomjali mteja katika viwango vya juu, hivyo kuwawezesha wateja wetu kuunganishwa na mtandao katika sehemu nyingi zaidi kuliko ilivyokuwa mwanzoni,” alisema Marcelo Aleman, Meneja Mkuu wa Tigo. “Uboreshaji huu utatuwezesha kuhudumia wateja wetu wengi na kutatua matatizo yoyote ya kimtandao kwa urahisi zaidi na kutoa huduma mpya kwa wateja wetu wa sasa na wateja wapya kwa haraka zaidi,” alisema. 

Kutokana na kwamba uboreshaji huo utaendelea huku huduma za simu zikiendelea kutolewa, wateja wanaweza kupata usumbufu kidogo katika siku chache zijazo lakini watandelea kupata huduma zote za Tigo kama kawaida. Jerome Albou, Afisa Ufundi Mkuu wa Tigo alisema: “kazi zinazohusiana na maboresho haya zitafanyika zaidi nyakati za saa 6 usiku mpaka saa 12 asubuhi ili kupunguza usumbufu kwa wateja wetu. Lakini pia inawezekana kwamba mitambo yetu ikayumba kidogo kutokana na maboresho haya na tumeandaa timu itakayokuwa tayari kutatua tatizo lolote pindi tu litakapojitokeza.

Kwa usumbufu wowote utakaojitokeza katika huduma zetu, wateja wanaweza kuwasiliana nasi kwa facebook kupitia (facebook.com/TigoTanzania), Twitter (@Tigo_TZ), barua – pepe (customercare@tigo.co.tz), kituo chochote cha huduma kwa wateja Tanzania, au kwa kupiga simu namba za msaada kwa wateja 100 au 0713 800 800. Tigo inapenda kuwakumbusha wateja wake kusajili namba zao kwa kutembelea kituo chochote cha huduma kwa wateja vilivyopo kote nchini Tanzania.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

1 comments:

  1. Sasa nafurahi tigo kuwa na lengo zuri lakutatua shida zetu. Lakini sisi tuliofamiwa na hakasi tusaidiwe upesi wawajibike watu then hela zirudishwe

    ReplyDelete