Katika pita pita za Kajunason Blog imeweza kupata baadhi ya picha katika maeneo mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam ikiwa ni siku ya tatu tokea mvua zianze kunyesha na kusababisha mafuriko ya makali pamoja na kuua watu wapatao 13 na wengi wao kukosa makazi. Hapa ni maeneo ya Myfair, Mikocheni ambapo barabara ilikuwa bado imejaa maji.
Haya ni maeneo ya daraja la Salender ambapo jana palikuwa pamejaa maji japo upande wa pili panapitika upande mmoja kutokana na kumeguka kwa daraja. 
  ...bado hali hairidhishi maeneo ya Jangwani, watu wanajaribu kuendelea kutoa viti vyao
 ...Maji bado yamejaa katika uwanja wa Kaunda, unaomilikiwa na Club ya Yanga.
 ...Heka heka bado zinaendelea
Mzee akijaribu kuokoa friji lake huku akiwa amezama maeneo ya Uwanja wa Kaunda jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Goodluck ole – Medeye (katikati mwenye miwani) akiongozana na viongozi wengine wa wizara yake mara baada ya kutembelea eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam.
...ilikuwa ni mshike mshike kila mmoja akihangaika pa kwenda
Akina mama wakijaribu kukusanya vyombo vyao
Vyombo vikiwa vimekusanywa huku hawajui pa kwenda
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Goodluck ole – Medeye (Wa kwanza kushoto mwenye miwani) akiongea na akina mama waliokuwa wamekusanya vitu vyao hawajui pa kwenda kutokana na nyumba zao kuzama kwenye maji.
...Wengine nao walikuwa wakihama kimya kimya...
...magondoro yakiwa yameanikwa
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Goodluck ole – Medeye (kushoto) akiangalia jinsi vijana walivyokuwa wamekaa wakijadili pa kwenda.
...Kituo cha polisi Jangwani jijini Dar es Salaam nacho kulikuwa kimejaa maji huku pembeni nyumba ikiwa inapangishwa.
Nyumba inapangishwa
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Goodluck ole – Medeye (katikati mwenye miwani) akiongea na muadhirika Bw. Seif na mkewe ambao wao nyumba yao imejaa maji na hakuna kitu walichoweza kuokoa zaidi ya maisha yao.
Hivi vitu vya Bw. Seif vikiwa vimejaa maji
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Goodluck ole – Medeye akiongea na Bw. Seif.
...barabara ilikuwa imejaa maji ya kutosha
...sehemu ya Jangwani upande wa chini maji yalikuwa bado yamejaa nyumba zinaelea
...nyumba zimeharibika vibaya
...magari nayo yalikuwa yameharibika
...kila mmoja alikuwa yuko katika harakati za kuhama
...umati wa watu ukiwa unasubiri kuvuka japo kila mtu ambayye alikuwa akivuka alitozwa tshs.200/= na vijana ambao wao walidai ndiyo wametengeneza daraja hilo la muda.
...daraja lenyewe la muda likuwa ni hili hapa unatozwa tshs.200/= ndipo uvuke, huna unabaki ng'ambo.
...maji yalikuwa bado yamejaa
...Kiukweli kama ulikuwa ni mtu mwenye roho nyepesi usingeweza kufika eneo hili bila kulia machozi.
Huu ni upande wa pili wa mtu Jangwani, maji haya ndiyo yalikuwa yakielekea Baharini kupitia Daraja la Salender jijini Dar es Salaam.
...mwenyewe walishaondoka
Watu wakijaribu kuhamisha vitu vyao
Hali ilikuwa ni mbaya sanaaaa
...barabara ya Kawawa ilikuwa ni nyeupeee
Napo Kigogo mwisho hali ilikuwa kama unavyoinona mwenyewe
...huku ni Kigogo, jijini Dar angalia jinsi barabara ilivyoharibika
...jamaa akiwa amekusanya vitu vyake huku hajui pa kwenda
...barabara ya Kigogo kupitia Loyola angalia jinsi ilivyomeguka
kila mto ulikuwa umejaa vya kutosha
Mali zilivyoharibika
...Eneo hili la barabara ya Kigogo kupitia Loyoya mpaka Mabibo jijini Dar lilikuwa limejaa maji vya kutosha jambo ambali liliwafanya wakazi wa huku kukaa majumbani kwao bila kutoka. Leo panaonekana salama baada ya mvua kukatika kunyesha.
...Wakazi wa Kigogo nao walikuwa kwenye harakati za kuhama makazi yao.
Eneo la Mabibo mwisho napo jana palikuwa hapafai.
Huu ni mto wa Tabata External kama unavyouona umejaa maji ambapo ilisababisha relini palikuwa hapapitiki kutokana na kufulika.
Bar nayo ilikuwa imejaa maji
Eneo hili la reli lote nalo lililkuwa limejaa maji.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: