Rais
Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na viongozi wa nchi mbalimbali
waliohudhuria katika maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania
yanayofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam mchana huu
hapa akisalimiana na Rais wa Namibia Mheshimiwa Hifikepunye Pohamba.
FULLSHANGWE inakumuvuzishia moja kwa moja matukio ya maadhimisho hayo
kutoka kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam ili kukujuza mambo
mbalimbali yaliyojiri katika sherehe hizo.
Rais
Jakaya Kikwete akielekea Jukwaa kuu mara baada ya kukagua gwaride
katika sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Tanzania kwenye uwanja wa Uhuru
huku akiwa ameongoza na na Mkuu wa Majeshi nchini Jenerari Davis
Mwamunyange.Rais
Jakaya Kikwete akikagua vikosi vya ulinzi na usalama wakati wa
maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania kikosi hiki ni cha Jeshi la
Wananchi wanawake
Rais jakaya Kikwete akipokea heshima wakati mizinga ikipigwa na jeshi la wananchi kwa heshima ya Rais.
Hiki
ni kikosi cha Jeshi la wananchi wanamaji kikiwa tayari kutoa heshima
kwa amiri jeshi mkuu na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tamnzania Dk.
Jakaya Kikwete.
Rais
Dk. Jakaya Kikwete akipungia mkono wananchi wakati alipowasili kwenye
uwanja wa uhuru kwa ajili ya kuongoza sherehe za miaka 50 ya Tanzania.
Msafara
wa Rais Dk Jakaya Kikwete ukiwasili kwenye uwanja wa Uhuru tayari kwa
kuongoza watanzania katika sherehe za miaka 50 ya Tanzania.
Walinzi wa rais walikuwa kivutio katika sherehe.wakati msafara wa Rais Dk. Jakaya Kikwete ukiwasili katika uwanja wa Uhuru leo.
---
Shukrani zangu zikuendee Fullshangwe Blog (www.fullshangwe.blogspot.com) kwa kazi ambayo umeifanya kwa vile mimi nilikosa kitambulisho na nilifuatilia sana ila ilishindikana mpaka hatua za mwisho.
Toa Maoni Yako:
0 comments: