Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza kuwahutubia wananchi waliohudhuria mkesha wa sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru, zilizofanyika usiku wa kuamkia leo Desemba 8 kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamanda Suleiman Koba, baada ya kuwasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo kuhudhuria Mkesha wa Sherehe za Maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
- Baadhi ya Viongozi wa Kisiasa na wananchi waliohudhuria sherehe hizo.
Wasanii wa Kundi la Taarab la Culture kutoka Zanzibar, wakitoa burudani jukwani.
Wanenguaji wa Bendi ya TOT Plus, wakishambulia jukwaa wakati wa mkesha wa sherehe hizo.
Rapa na mwimbaji wa Bendi ya TOT Plus, Jua Kali, akighani rap zake jukwaani wakati wa mkesha wa sherehe hizo.
Wasanii wa Kikundi cha Sanaa cha JKT Mgulani, wakishambulia jukwaa kwa kucheza ngoma ya Bugobogobo ya Kabila la Wasukuma, wakati wa sherehe hizo.
Baadhi ya Vijana waliohudhuria sherehe hizo
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: