Na Mwandishi Wetu

MLEZI wa mchezo wa ngumi 'Masimbwi 'Mawe' Tanzania kamanda wa Polisi wa kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova anatarajia kuwa mgeni rasmi katika pamabano kati ya Rashid Matumla ‘Snake Man’ na Maneno Osward ‘Mtambo wa Gongo’ linalotarajia kufanyika Desemba 25 katika ukumbi wa Heinken, Mtoni Kijichi Dar es Salaam.

Pambano hilo lisilo la ubingwa linatarajia kuwa katika uzito wa middle weihgt raundi 10.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Maneno Osward alisema atahakikisha anamtwanga mpunzani wake ili kufuta machungu ya kumzidi kwa pointi katika pambano lao walilocheza hivi karibuni.

"Matumla alinizidi kwa pointi sasa nataka kumonyesha kama ninauwezo wa kumuangusha katika hatua za awali za pambano letu kwani nimejiandaa na bado naendelea kujifua kwa ajili ya pambano hilo," alisema Maneno.

Naye kwa upande wake Rashid alisema, anaendelea kujifua ili kuweza kuwapa raha mashabiki wake ikiwa na kuwapa zawadi ya Christimas kwa kumtwanga kwa mara nyingine Maneno.

"Ushindi wangu ndio utakuwa zawadi kwa mashabiki wangu kwani sinachazaidi cha kuwapa," alisema Rashid.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Adios Promotion, Shabani Adios 'mwayamwaya' ambaye ndiye muandaaji wa pambano hilo, alisema kabla ya kufanyika kwa pambano hilo mabondia hao watapima vipimo mbalimbali vikiwemo ukimwi na madawa ya kuongeza nguvu ili kuweza kuwatayari kwa ajili ya mpambano.

Mapambano ya utangulizi yatakuwa kati ya mabondia Venas Mponji atakayezichapa na Tumaini Maguno 'SMG' na bondia  Rashidi Ally atazichapa na Kulwa Mbuchi, Selemani Jumanne na Ibrahimu Madeusi wakati Shabani Zunga atavaana na Mohamedi Kashinde, na bondia Sweet Kalulu na Saleh Mtalekwa

Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: