MAGWIJI wa soka Ghana, Asante Kotoko sasa itacheza na timu ya Simba peke yake  katika mechi maalum ya kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.

Awali Asante Kotoko ilipanga kucheza na timu ya kombaini ya Simba na Yanga, hata hivyo Yanga wakabadili maamuzi na kuamua kutotoa wachezaji katika mchi hiyo muhimu ya historia.

Mkurugenzi wa kampuni ya Future Century, Alberto Albano alisema jana kuwa hakuna taarifa za kimaandishi ambazo timu hiyo ya Jangwani imetoa  kwao zaidi ya kutumia vyombo vya habari pekee.

“Ni taarifa ambazo hazikuwa rasmi, lakini kutokana na hali ilivyokuwa, tumeamua bora kuachana nao na siku hiyo kuwapa nafasi Simba kuonyesha uwezo wao ikiwa pamoja na kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Tanzania Bara,” alisema Albano.

Alisema kuwa maandalizi yamekamilika na Asante Kotoko inatarajia kuwasili nchini kesho kwa ajili ya mchezo huo ambao umedhaminiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PPF. Wadhamini wengine ni….
Abano pia alisema kuwa mchezo huo ni sehemu ya kumtambulisha kwa mara ya kwanza kocha mkuu wa Simba, Mserbia,  Cirkovic Milovan ambaye amechukua mikopa ya kocha wa Uganda, Moses Basena.

Viingilio vya mchezo huo ni sh. 30,000 for VIP A, shs. 15,000 (VIP B), Shs. 10,000 for VIP C and shs. 7,000 kwa viti vya orange. Viti vya kijana ni shs. 3.000.

Tiketi kwa ajili ya mchezo huo zinapatikana Steers, Big Bon,  Oilcom, Benjamini Mkapa secondary school, Zizou fashion na Uwanja wa Taifa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: