Ndugu wa maheremu wakiomboleza kwa kulia.

Msafara ukiongozwa na mjukuu wa marehemu kuelekea kanisani kwa ajili ya misa.
Msafara ukiingia kanisani kwa ajili misa takatifu.
Padre akibariki mwili wa marehemu B. Felista Kashaija
Mama Ketau ambaye alikuwa ni rafiki na mfanyakazi mwenzake na marehemu akisoma neno.

Masista kutoka jimboni nao walihudhuria misa.
Ndugu, jamaa na marafiki wakitoa heshima zao za mwisho.




Padre akitoa heshima za mwisho tayari kwa kwenda kuzika.
Mwili wa marehemu ukingizwa makaburini.
Mwili wa marehemu ukiwa tayari kwa kuzikwa.
Wakisaidia kuuingiza mwili wa marehemu kaburini.
...ndugu, jamaa na marafiki wakiweka udongo, ishara ya kushiriki mazishi.
Mtoto wa marehemu akiweka shada la maua
Mme wa maheremu akiweka shada la maua
...masista nao waliwakilisha
Padre nae aliweka
Kaka wa marehemu akiweka shada la maua
Wajukuu wakiwa wameshika msalaba na picha za marehemu
HISTORIA YA MAHEREMU BI FELISTA KASHAIJA

Alizaliwa mwaka 1949 katika kijiji cha Kabare wilayani Muleba mkoani Kagera, alipata elimu ya msingi mkoani Kagera, elimu ya sekondari mkoani Tabora.

Alikuwa mwajiri wa serikali katika Wizara mbalimbali kwa nyakati tofauti mpaka alipostaafu mwaka jana 2010 akiwa mfanyakazi wa Wizara ya Viwanda na Biashara. Marehemu alikuwa mstari wa mbele katika kumtumikia Mungu katika kanisa la Mtoni Roman Cathoric. Alishika nyazifa mbali mbali kwenye Kamati ya Uchumi na Mipango na Katibu wa WAWATA kwa muda mrefu. Jimboni alikuwa katika Kamati ya Tegemeza Jimbo bila kusahau alikuwa Mwenyekiti wa Jumuiya na Kiongozi katika kanda pia mlezi wa Vijana.

Marehemu alipatwa na ajali siku ya jumapili tarehe 27.110.2011 maeneo ya Kurasini (round about shule ya sekondari Jitegemee) akiwa safarini kujerea nyumbani kwake alipokimbizwa hospitali ya Taifa Muhimbili na hali yake iliendelea kuwa mbaya hadi umauti ulipomfikia siku ya jumatano tarehe 30.11.2011 jioni saa 12. Marehemu ameacha watoto 2 na wajukuu 4

MUNGU ALITOA NA MUNGU AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE

AMINA.

N:B Kajunason blog inapenda kuwapa pole wafiwa na Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi..
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: